WANAWAKE wengi duniani bado wananyanyaswa kijinsia kwa sababu za kijamii, kiuchumi na kipato licha ya kuwepo kwa elimu kuhusu haki zao.


Mwanamama Ester Charles ambaye ni mkazi wa Mwambani wilayani Ilemela ametelekezwa na mumewe aliyetajwa kwa jina la Albinus na kubakizwa na watoto wawili wadogo wanaohitaji uangalizi na usimamizi. Pichani mwanamama Ester akiwa na mtoto wake mdogo anayetaabika na ugonjwa wa kupooza. 



KWA UFUPI

Mumewake alipopata mwanamke mwingine alihama nyumba aliyokuwa akiishi na mama huyu na kupanga eneo jingine kabisa bila kuikumbuka familia yake katika matumizi na mahitaji muhimu.
Alipomfikisha mumewe huyo mbele ya mikono ya Sheria alikubali kutoa huduma lakini ndani ya kipindi kifupi alitorokea kusikojulikana.
Amefika kuomba msaada toka kwa wasamalia wema watakaoguswa na simulizi yake. BOFYA PLAY KUSIKILIZA. 
Hali ya afya ya kwa mtoto Jr. Albinus si ya kuridhisha na haijafahamika nini kinachomsibu kwani bado hajafika hospitali kupata matibabu ya kina. Mtoto huyu pichani hawezi kutembea, hawezi kuzungumza kwa ufasaha wala kukaa, zaidi ya kulala tu muda wote.


CHANGAMOTO ALIZONAZO MAMA ESTER.

Hana pesa kwaajili ya chakula cha watoto.
Hana nguo kwaajili ya kuwavisha watoto na yeye binafsi.
Anadaiwa pesa ya kulipia nyumba anayoishi kiasi kwamba mwenye nyumba anataka kumfukuza.
Amejaribu kuomba kazi kwenye kaya mbalimbali na kukosa, akipewa majibu kuwa hawezi kuajiriwa akiwa na watoto (atashindwa kufanya majukumu ya mwajiri) naye hana sehemu ya kuwahifadhi iwe ndugu au majirani.
Jeh! Umeguswa tafadhali wasiliananaye kupitia namba 0753804881.

MUNGU AWABARIKI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. People should learn to take responsibility of their actions. If u like 'uroda' then u should learn to live the consequences. U were not 'raped' so I cannot help u. U were having fun. If I help u the next time you will tell me u have twins who need help! Sorry for being negative but I can't help u! I'm a practical guy.

    ReplyDelete
  2. Mdau hapo juu, kama ni kutoa msaada hutakuwa umemsaidia huyu mama, utakuwa umemsaidia mtoto huyu ambaye hana hatia yeyote. Amezaliwa na kujikuta katika hali hiyo. Wanazaliwa watoto mapacha wengi, watoto wenye ulemavu wa aina moja au nyingine, ama wagonjwa wa magonjwa yasiyotibika, na hii haijalishi kama wazazi wao wana uwezo au la. Kwa taarifa yako hakuna mzazi hata mmoja anaetegemea atazaa mtoto katika hali hiyo. Hiyo ndio mipango ya Mwenyezi Mungu, na by nature alivyotuumba tuzaliane, na hakusema tuzaliane wakati tu tukiwa matajiri. Na ikitokea bahati mbaya kama ilivyo kwa huyu mtoto, ni wajibu kusaidia. Hili lingeweza kumpata yeyote, hata kwako wewe ndugu..Uombe Mungu tu kama hujazaa, lisikutokee, na kama umemaliza kuzaa, basi laweza kutokea hata kwa wajukuu. Waswahili husema usitukane mkunga na uzazi ungalipo.. And there is a saying "It is better not to say anything, if you have nothing good to say to a fellow human being"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...