Tunayo furaha kukujulisheni kuwa taasisi ya
Boko Beach Veterans Sports Club (BBV) itaandaa maonyesho ya kimataifa ya vipaji
vya mpira wa miguu kwa vijana wa mashuleni na vyuoni, kuanzia tarehe 19 had 21
kwenye uwanja wao wa kisasa ulioko maeneo ya Boko, Kinondoni , Dar es
salaam.
Maonyesho haya ni nafasi dhahiri
kwa vijana wenye vipaji vya kusakata mpira wa miguu, wavulana kwa wasichana,
kucheza soka nchini Marekani huku wakisoma katika vyuo vya nchini humo kwa
kulipiwa gharama zote. Makocha wapatao watatu (3) kutoka katika chuo kikuu cha
Alabama, Chuo kikuu cha Martin Methodist and chuo kikuu cha Lindsey Wilson
wamesha thibitisha kushiriki na tunawategemea kufika tarehe 15 Desemba 2014.
Pia yanawapa vijana wa
kitanzania nafasi ya kupata udhamini wa kusoma katika vyuo vikuu vya Marekani.
Ni mpango wa ufadhili ambao unawaunganisha vijana wa kitanzania wenye ndoto ya
kucheza mpira pamoja na kusoma na ulimwengu mzima. Boko Beach Veterans Sports
Club (BBV) tayari tumekwisha alike shule
mbali mbali kuleta washiriki.
Pamoja na kuwa na wachezaji wengi walio
wahi kuwika Tanzania, ni wacheche sana wameweza kuwa na maisha mazuri baada ya kustaafu kucheza, sababu kubwa ikiwa ukosefu wa elimu bora.
BBV inakukaribisha sana kushiriki katika maonyesho haya ya
kwanza nay a aina yake na yenye mweleleo wa kuleta faida kubwa binafsi kwa
washiriki na kwa taifa kwa ujumla. BBV ina nia ya kuandaa maonyesho haya kila
mwaka ikiwa ni mchango wake katika kampeini za TFF na serikali ya kuinua
kiwango cha soka nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...