Na Ripota Wetu,Dar
MASTAA nane wa klabu ya Msimbazi wamekacha timu hiyo iliyoandoka leo kwenda
Zanzibar kwa kile wanachoshinikiza kulipwa fedha zao.
Habari za kuaminika zinasema kuwa mastaa nane wa klabu hiyo wameingia mitini
wakiwemo waganda watano na wabongo watatu mpaka hapo watakapomaliziwa fedha zao
za usajili.
Wabongo waliokacha timu hiyo ni Shaban Kisiga, Jonas Mkude na Ivo Mapunda hata hivyo
kocha msaidizi wa timu hiyo Seleman Matola jana alikiri kutokuwepo kwenye kikosi chake
wachezaji hao na kuweka wazi kuwa Ivo amekwenda Mbeya kwenye arobaini ya mama
yake mzazi aliyefariki hivi karibuni, huku akiwa hana taarifa za Kisiga na Mkude.
Pia mbali na wachezaji hao wa kibongo, wachezaji waganda ambao wameingia mitini ni
Emmanuel Okwi ambaye alikuwa wa kwanza kutimka mara baada ya kichapo cha bao 1-0
dhidi ya Kagara. Wengine ni Joseph Owino, Dan Sserunkuma, Juuko
Murshid na Simon Sserunkuma.
"Ninaondoka na wachezaji wachache, nina taarifa za Ivo tu ambaye ameenda kwenye
harobaini ya mama yake, wengine sina taarifa zao." alisema Matola ambaye hata hivyo
ameaidi kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Kikosi hicho cha Simba kimeondoka leo asubuhi kuelekea Zanzibar tayari kwa michuano
ya Kombe la Mapinduzi itakayoanza kutimua vumbi keshoJanuari Mosi hadi Januari 13
kwenye uwanja wa Aman visiwani Zanzibar.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili Zakaria Hanspope alipotafutwa kuzungumzia suala hilo
alisema kwa kifupi "Nipo Iringa, sijui chochote kinachoendelea Simba kwa sasa, hayo
mambo waulizeni viongozi waliopo huko, mi mwenyewe nasikia tu lakini sijui chochote."
Mwenyekiti wa Simba Evans Aveva hakupatikana kuzungumzia suala hilo, hata hivyo
mmoja wa viongozi wa klabu hiyo aliiambia Mwananchi kuwa wachezaji hao waliondoka
kwa vile Simba hawakuwa na uhakika wa kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi.
"Unajua barua ya kuthibitisha yenyewe imetumwa juzi tu, hatukuwa na uhakika wa
kushiriki ndio maana tuliwaruhusu wachezaji kuondoka na warudi tarehe moja, wote wana
ruhusa maalum."alisema mmoja wa viongozi wa wekundu hao wa Msimbazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...