Ankal Michuzi akimpongeza Binti yake Zahra wakati wa hafla ya Maulid ya Kumpongeza baada ya kulamba Nondozz yake ya kwanza ya Biashara na Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dodoma hivi karibuni.Hafla hii imefanyika jana Nyumbani kwa Kaka wa Ankal,Tabata Kimanga jijini Dar es salaam.
 Baba Mkubwa wa Zahra,Ismail Michuzi akiongoza dua ya kuwakumbuka ndugu waliotangulia mbele ya haki kabla ya shereha ya Maulid ya kumpongeza Binti Zahra alielamba Nondozz yake ya Biashara na Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dodoma,hivi karibuni.Kulia ni Ankal.
 Ankal akiwa na Wanawe,Ramadhan (pili kushoto),Zahra (kulia),Karim (kushoto) na Sellah (alie na Ankal) wakati wa hafla ya Maulid ya kumpoza Zahra alielamba Nondozz yake ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Dodoma hivi karibuni.Hafla hii ilifanyika Tabata kwa Kaka wa Ankal ambaye ni Baba Mkubwa wa kina Zahra.
 Ankal Michuzi (shoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wanafamilia wakati wa hafla ya Maulid ya kumpongeza binti yao,Zahra (kati) baada ya kulamba Nondozz yake ya kwanza ya Biashara na Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dodoma hivi karibuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Maa Shaa Allah hongera tena Bi Zahra kwa kuhitimu masomo yako ya Nondozz. Nakuombea Allah akufanyie wepesi katika safari yako ya maisha, Amin. Hongera sana Ankal kwa familia bora Maa Shaa Allah. Ukerewe tumekosa Maulid kwa hakika ilifana sana.
    Mariam.M
    UK

    ReplyDelete
  2. Hongera sana umekuza na umedegreesha pia..congratulations bi Zahra.

    mdau wa ukerewe

    ReplyDelete
  3. Ankal na familia yako yako Hogereni sana kwa kumsomesha na mkumpa malezi bora bint yenu Zahra.Pia pongezi na Hongera kwako Bi.Zahra kwa kujitahidi na kufanikiwa katika masomo tukuombea kwa mwenyezi Mungu azidi kukuongoza uapate mafanikio zaidi .
    wadau FFU-Ughaibuni

    ReplyDelete
  4. Hongera sana Bi.Zahra kwa kuhitimu inshallah Mwenyezi Mungu akupe wepesi juu ya hatua nyngine inayofata ya masomo...nakupongeza sana My bro Michuzi kwa ulichokifanya hivyo ndivyo tunavyotakiwa waislam kuwafanyia watoto wetu wanapofanya vizuri badala ya kuweka rusha roho,kijamvi wewe ukaona ufanyae kisomo safi sana kaka Mungu atakulipa juu ya hili inshallah

    ReplyDelete
  5. Ankal umetufurahisha saaaaaana! Wengine hapo wangeandaa miparty na vileo. Weye umeamua kumrejea Raabana. Huo ni mfano wa kuigwa wallahi

    ReplyDelete
  6. Sikutegemea ankal ukafanza jambo hili. Maulid baada ya binti kula nonodozz ni thawab tosha

    ReplyDelete
  7. khaaaa,,,bi Zahra ni ankal mtupu hii ni pure photocopy,..hongera sana bi, Zahra mungu akuongoze huko kwingineko pia...ankal hongera pia kwa kukuza na kusomesha binti yetu you are one of the few to do that...akitaka kuongeza na ka masters niko tayari kumsaidia huku oxford...hongera sana bi Zahra.

    Mdau wa Oxford.

    ReplyDelete
  8. AMAZINGLY BEAUTIFUL FAMILY, CONGRATS MICHUZI.

    ReplyDelete
  9. Mi-stew na Bintiyo mmefanana kweli, pua ya binti ni yako hiyo! ndo maana wazee wa zamani wakimwangalia mtoto tu wanajua huyu wa kwako au umebambikiwa, hakuna hata haja ya DNA!

    ReplyDelete

  10. Asalaam alaykhum wajina!

    1. Hongera sana Michuzi kwa kumfanyia maulid Ankal Zahra ni jambo jema sana mbele ya Allah sisi binadamu si kitu.

    2. Hongera sana sanaaaaa Ankal Zahra kwa juhudi yako binafsi leo umemfanya wajina ankal Michuzi kutembea kifua mbele ni fahari kubwa sana kwako na kwa wazazi wako juhudi siku zote huwa inalipa.

    3. Ankal Zahra Mola akujaalie huu uwe mwanzo wa mafanikio kimaisha na kielimu lenga kufika mbali zaidi usiishie hapa elimu ni kila kitu katika maisha ya sasa pambana weka malengo utafika kwa uwezo wa Allah.

    HONGERA SANA ANKAL ISSA MICHUZI NA FAMILIA YAKO MOLA AWAJAALIE MAISHA MAREFU YA FURAHA NA AMANI AMEEN

    Executive chef Issa Kapande

    ReplyDelete
  11. David KyunguDecember 09, 2014

    Ndaga Mnyambala, Hongera sana kwa hatua uliyofikia! Ila usichoke, kwani Mapambano bado yanaendelea! Tuko pamoja. (Dav Kyungu)

    ReplyDelete
  12. Kwa sura hizo za watoto Ankal hapo hakuna ujanja uliofanyiwa!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...