Katika mahafali ya 13 katika chuo kikuu Mzumbe yaliyofanyika Ijumaa katika kampasi kuu Mzumbe, Morogoro mdau Peter Samanya Msacky alilamba nondozzz ya Uzamili ya Uhasibu na Fedha (MSc in Accounting and Finance) ya Chuo Kikuu Mzumbe (MU).
Bwana Msacky akipongezwa na mke wake mpendwa Judith mara tu baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamili
Glad akimpongeza baba yake kwa mafanikio aliyopata kwa kutunukiwa Shahada ya Uzamili, anaonekana akimhakikishia baba yake kuwa hata yeye atajitahidi katika mafunzo yake ili kufikia ndoto yake.
Mdau Msacky akipongezana na rafiki yake Bwana Mawalla baada ya kutunukiwa shahada za Uzamili
Picha ya pamoja ya familia ya bwana na bibi Peter Msacky baada ya tafrija fupi iliyofanyika katika viwanja vya Magadu mjini Morogoro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...