Kaimu Mwenyekiti wa umoja wa wamiliki wa shule na vyuo
binafsi(TAMONGSCO),Bw.Leonard Mao(Kushoto) akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya maamuzi ya Serikali kutatua
mgogoro wa TAMONGCO,kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa umoja huo,Bw.Mrinde
K.Mnzava.
Na
Bakari Issa,Dar es Salaam.
Uongozi wa shirikisho la wamiliki
na mameneja wa shule na vyuo visivyo vya serikali(TAMONGSCO) lililokuwa katika mgogoro na kikundi cha
waliokuwa viongozi wa kitaifa(National Office Bearers) kilichofanya hujuma za
kutaka kuifanya TAMONGSCO kuwa mali yao binafsi.
Mara baada ya Katiba kufanyiwa marekebisho kumi(10) na
mkutano mkuu(AGM) uliofanyika Mbeya katika ukumbi wa Benjamin William Mkapa,AGM
iliagiza kamati kuu ya Taifa (NEC) kuingiza marekebisho hayo kwenye katiba na
kuipeleka kwa msajili wa asasi za kiraia(CSO) ambaye ni Wizara ya Mambo ya
ndani ya nchi.
Akithibitisha uongozi wa
shirikisho hilo,Kaimu Mwenyekiti wa Umoja wa wamiliki na mameneja wa shule na vyuo visivyo vya serikali,Bw.Leonard Mao
amesema uongozi uliokuwa madarakani ndiyo sahihi pamoja na Katiba iliyopita na
kuongeza kuwa wanaosema katiba na uongozi uliochaguliwa sio sahihi hao sio
wanachama wetu na kuagiza waache kabisa.
“Uongozi wa waliotaka kuchakachua
katiba ya umoja huu,muda wao umekwisha na uongozi uliochaguliwa ndio
uongozi sahihi pamoja na katiba iliyopendekezwa,na wanaosema uongozi pamoja na katiba iliyopendekezwa sio
halali hao si wanachama wetu na waache kabisa”,alisema Bw.Mao
Naye Kaimu Mwenyekiti wa umoja
huo,Bw.Mrinde Mnzava alisema kuwa umoja
huo ndiyo unaoongoza kutoa wanafunzi bora nchini na kuisaidia Serikali kuweka vizuri
miundombinu ya shule pamoja na vyuo.
Aidha amesema umoja huo utafanya kikao
mkoani Dodoma ili
kuteua nafasi ya Mwenyekiti ambayo imeachwa wazi na aliyekuwa Mwenyekiti
Kitaifa,Ally Hassan Mwanakatwe aliyefariki dunia.
“Umoja huu unalisaidia Taifa katika kutoa wanafunzi bora
na kuipa changamoto Serikali kuboresha miundombinu ya shule na vyuo kwa ujumla
na tunatarajia kufanya kikao mkoani Dodoma
ili kumchagua Mwenyekiti mpya kitaifa”,alieleza
Mnzava
Pia Naibu Katibu Mkuu wa
TAMONGSCO,Bw.Chelestino Mofuga alitoa pongezi kwa Serikali
kwa kuweza kusuruhisha suala hilo ambalo kwa sasa limefika mwisho na
kuhakikisha kuwa mgogoro huo haupo tena.
“Pongezi kwa Serikali kwa suala
hili,lakini wamiliki wa shule binafsi tunakabiliwa na changamoto ya lugha
katika kufundishia katika shule pamoja na vyuo”,alimaliza kusema Mofuga
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...