Mheshimiwa Dkt Pindi Chana (Mb.), Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Njombe na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Tarehe 10-12/12/2014 alifanya ziara ya kikazi ya chama Mkoani Njombe kwa kushiriki katika kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Katika ziara hiyo pamoja na shughuli nyingine Mhe. Mbunge aliwanadi wagombea uongozi kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji vya Mkoa wa Njombe. Kupitia mikutano hiyo ya kampeni wagombea walipata fursa ya kueleza sera na ahadi zao kwa wananchi, endapo watawapa ridhaa ya kuwaongoza.
Mhe. Dkt. Pindi Chana, akiwatambulisha wagombea wa Uongozi kwa Tiketi ya CCM wa Serikali ya Kijiji cha Mbugani – Ludewa, Njombe, wakati wa mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Mbugani, Wilayani Ludewa.
Mhe. Dkt. Pindi Chana, akiwatambulisha wagombea wa Uongozi kwa Tiketi ya CCM wa Mtaa wa Kihesya - Njombe, wakati wa mkutano uliofanyika Njombe Mjini.
Mhe. Dkt. Pindi Chana, akiwatambulisha wagombea wa Uongozi kwa Tiketi ya CCM wa Serikali ya Kijiji cha Mavanga – Ludewa, Njombe, wakati wa mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Mavanga, Wilayani Ludewa.
Mhe. Dkt. Pindi Chana, akiwatambulisha wagombea wa Uongozi kwa Tiketi ya CCM wa Mtaa wa Kwivaha - Njombe, wakati wa mkutano uliofanyika Njombe Mjini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...