Walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini
unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF wameanza utekelezaji wa
miradi ya ajira za muda na kisha kulipwa ujira katika miradi wanayoibua kwenye
maeneo yao .
Walengwa wa vijiji kadhaa vilivyoko kwenye
Mpango huo kikiwemo kile cha Mzuri na Kijini vilivyoko katika eneo la
Makunduchi mkoa wa Kusini Unguja wameanza kutengeneza barabara yenye urefu wa
zaidi ya kilometa moja na vitalu vya miche ya miti ya asili na matunda katika
eneo lao na kisha kulipwa fedha chini ya utaratibu ulioandaliwa na TASAF ambao
ni moja ya mkakati wa kuwaongezea kipato
walengwa na kupambana na umaskini.
Akizungumza na timu ya waandishi wa habari
waliotembelea eneo hilo Sheha wa eneo hilo Bwana Mwita Masemo Makungu
amebainisha kuwa mpango huo umeitikiwa vizuri na walengwa wa Mpango wa kunusuru
kaya maskini katika eneo hilo na kuwa jitihada hizo za TASAF zimeamsha ari ya
wananchi kujiletea maendeleo kwenye maeneo yao na kupunguza kero ya barabara
iliyokuwa inawakabili.
Hata hivyo Bwana Makungu amesema pamoja na
ushiriki wa wananchi kwenye kazi hiyo kupitia mpango wa ajira za muda bado
wananchi hao wanakabiliwa na tatizo la vifaa na utaalamu hususani katika ujenzi
wa barabara ambao unahitaji vifaa vizito ambavyo havipo kwenye maeneo yao na
hivyo kuomba serikali kuona namna ya kukamilisha kazi hiyo.
Zifuatazo ni baadhi ya picha za walengwa wa PSSN
katika wilaya ya Makunduchi mkoa wa Kusini Unguja wakishiriki katika kazi
kupitia ajira za muda PWP.
Kazi
ya ujenzi wa barabara katika kijiji cha Kijini -Makunduchi mkoa wa kusini
Unguja ambayo ni moja ya mkakati wa TASAF wa kuwaongezea kipato walengwa wa
Mpango wa kunusuru kaya maskini kupitia ajira ya muda PWP.
Baadhi
ya walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa na TASAF katika
kijiji cha Kijini Makunduchi mkoa wa kusini Unguja wakishiriki katika kazi za
ujenzi wa barabara kupitia mpango wa ajira za muda PWP.
Walengwa
wa mpango wa kunusuru kaya maskini katika eneo la Kijini Makunduchi mkoa wa
kusini Unguja wakiwa katika harakati za ujenzi wa barabara kupitia mpango wa
ajira za muda PWP kupitia TASAF.
Barabara
inayojengwa kupitia mpango wa ajira ya muda PWP ambapo walengwa wa Mpango wa Kunusuru
kaya maskini kupitia TASAF wakiwa katika eneo la mradi wa barabara yenye urefu
wa kilometa Moja .
Wakazi
wa kijiji cha Mzuri -Makunduchi mkoa wa Kusini Unguja wakiwa katika mradi wa
kitalu cha miti moja ya mradi ulioibuliwa na walengwa wenyewe kupitia PWP
unaoendeshwa na TASAF ambapo walengwa hulipwa fedha kwa kazi hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...