KAMPUNI ya Msama Video Productions
imetoa tamko kwamba mwaka huu wamejipanga vizuri kufikisha ujumbe wa
neon la Mungu katika Tamasha la Krismas kwani wanavifaa vipya na vya
kisasa vyenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi katika mazingira yoyote yale
na wafanyakazi wakutosha wenye weledi katika fani hiyo.
Akizungumza jijini Dar
, Meneja wa kitengo hicho, Alpha
Kigalla alieleza sababu za kufanikisha vilivyo katika tamasha hilo ni
kwa sababu ya umahiri wa watendaji wa kirengo hicho ndio chachu
itakayofanikisha kutekeleza ibada hiyo kwa waumini na mashabiki
watakaojitokeza katika Tamasha hilo.
Kigalla alitoa wito kwa wakazi wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kujitokeza kwa wingi kushuhudia kazi za kitengo hicho kilicho katika kampuni ya Msama kwani wana vifaa vya kisasa zaidi.
“Msama Video Productions ina vifaa vipya na vya kisasa zaidi na hata watendaji wake wako makini zaidi na utekelezaji wa kazi zao, hivyo wadau wa muziki nchini kujitokeza kufanikisha kazi zao,” alisema Kigalla.
Meneja huyo alisema wakazi wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kujiandaa na kazi bora za Msama Video Productions ambazo zitafanikishwa kupitia waimbaji mbalimbali wa muziki huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...