Askari polisi pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali ya mtaa kata ya Gongoni manispaa ya Tabora akiangalia mwili wa mwanaume mmoja ambaye ni Msusi katika moja ya Saloon za wanawake hapa manispaa ya Tabora inayofahamika kama HK.
Mwanaume huyo ambaye amefahamika kwa jina la Ramadhani amekutwa amefariki dunia akiwa chumbani katika nyumba ya kulala wageni inayofahamika kwa jina la SALAMA GUEST  HOUSE ambapo ilidaiwa kuwa alikuwa ameishi katika nyumba hiyo kwa muda wa siku tatu kabla ya kufikwa na umauti.
Mwili ukichukuliwa na Polisi  baada ya kuvunjwa mlango wa chumba katika  Guest House hiyo.
Dada huyu inasemekana kuwa ndiye alikuwa mpenzi wake marehemu huyo Ramadhani
Baadhi ya wananchi waliofika katika Guest house hiyo kushuhudia tukio hilo.
Hii ndio HK Saloon aliyokuwa akifanyia kazi msusi huyo maarufu wa nywele za akina mama ambapo kifo chake kimegubikwa na wimbi la utata kutokana na maelezo kuwa aliondoka Saloon hapo baada ya kufunga milango na kuelekea huko Guest house akiwa mzima wa afya.
Habari kwa hisani ya http://kapipij.blogspot.com/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. watanzania jamani kweli hatuna la kufanya na muda wetu. Pasitokee jambo mahali wat wanajazana, iwe ajali ya gari, moto, au kifo kama hiki. Yaani hao watu wamekusanyika hapo kwa manufaa gani hasa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...