Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akimkabidhi cheti mmoja ya
washiriki wa mafunzo ya D.H.I.S Osama Al
Zubair kutoka Sudan wakati wa kufunga
mafunzo hayo katika Hoteli ya Double Tree Nungwi, Kaskazini Unguja.
Mgeni rasmi katika ufungaji wa mafunzo ya D.H.I.S Mahmoud Thabit Kombo
akiwahutubia washiriki wa mafunzo hayo kutoka Nchi za Afrika, Marekani, Ujerumani
na Mashirika wahisani katika Hoteli ya Double Tree Nungwi.
Mratibu wa mafunzo ya mfumo wa ukusanyaji taarifa za Afya (D.H.I.S) Suleiman Salum Ali akieleza mafanikio ya mafunzo hayo yaliyofanyika Hoteli ya Double Tree Nungwi, wa kwanza (kulia) ni Profesa Kristin Braa kutoka Chuo Kikuu cha Oslo ambao ni waandaaji wa mafunzo hayo kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Wizara ya Afya Zanzibar. (kati) ni Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo aliefunga mafunzo hayo. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo zanzibar)
Washiriki wa mafunzo hayo
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo alipokuwa
akiyafunga mafunzo ya siku 10 yaliyofanyika Hoteli ya Double Tree Nungwi.
Mratibu wa mafunzo ya mfumo wa ukusanyaji taarifa za Afya Suleiman Salum Ali
akizungumza na waandishi wa Habari walioshiriki ufungaji wa mafunzo hayo katika
Hoteli ya Double Tree Nungwi.
Picha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo ya mfumo wa ukusanyaji taarifa za Afya
(D.H.I.S) wakiwa na mgeni rasmi katika kufunga mafunzo hayo Naibu Waziri wa
Afya Mahmoud Thabit Kombo katika Hoteli ya Double Tree Nungwi. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo zanzibar).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...