Meneja wa ATM na Kadi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Wambura John (kushoto) akiweka pesa kwa kutumia ATM katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya kuweka pesa (deposit) kwa kutumia mashine za ATM ya benki ya NBC jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati ni mteja wa benki hiyo, Francis Xavier na kulia ni Meneja Huduma za Jamii wa NBC, Irene Peter
Mteja wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Francis Xavier (kushoto) akiweka pesa (deposit) katika mashine ya ATM ya benki hiyo wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati ni Meneja wa ATM na Kadi wa NBC, Wambura John (katikati) na Meneja Huduma za Jamii wa benki hiyo, Irene Peter.

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma mpya ya kuweka fedha kwenye mashine za ATM jijini Dar es Salaam katika juhudi za benki hiyo kuboresha huduma za kifedha nchini.

Kuanzishwa kwa huduma hiyo kunathibitisha malengo ya benki hiyo ya kutoa huduma sahihi na ya wakati kwa wateja wake nchini nzima na huduma hii ya kuweka fedha kwenye mashine za ATM itakuwa ikipatikana masaa 24 kila siku.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. NBC BANK wakati mnaleta huduma hii ni wakati muafaka wa kujiuliza huduma zilizopo zina usalama gani? ba zinamlinda vipi mteja. HUO WIZI WA MTANDAO WA ATMS MMEWEZA KUUDHIBITI VIPI?

    ReplyDelete
  2. Mdau kweli kabisa...kulikuwa na uvumi wa hackers ukakanushwa, lakini matukio ya wateja kuibiwa fedha zao yanaongezeka. Kuna jamaa yangu amelizwa hela zote NBC Bank tarehe 25 na 26. Mbaya zaidi Bank hazina msaada pindi hela za mteja zinapoibwa. Utajaza fomu na kusubiri siku 45. Uwe na bahati zirudishwe kwa haraka.

    NBC BANK muwe sensitive

    ReplyDelete
  3. kama noti zimechakaa, basi sahau hii mashine haiwezi kupokea. Inapokea tu noti mpya. Ikikunjana tu, basi nongwa. Halafu vile vile itachukua muda mrefu kama unaweka milioni moja, itakuwa ni sawa na kumliza mtoto uji ndoo nzima.

    Mkulima

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...