Benki ya NMB leo imefungua tawi jipya maeneo ya Gongo la mboto- Dar es
Salaam tawi linalokadiriwa kuhudumia zaidi ya wateja 300 kwa siku. Tawi hili lipo
karibu na kituo cha dala dala cha Mzambarauni mkabala na kituo cha mafuta Oil
com.
Tawi hili linatoa huduma kwa wakazi wa Chanika,Pugu,Majohe,Kitunda,Mongo la
ndege na maeneo yote ya karibu.Vile vile huduma zote za kibenki zinapatikana
katika tawi hili zikiwamo ufunguzi wa akaunti mbali mbali,Huduma za mikopo
pamoja na huduma za kuweka na kutoa fedha.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Mhe. Raymond Mushi, akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la
NMB Gongo la Mboto . Kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya Dar e salaam – Bw. Salie Mlay na
kulia ni meneja wa NMB Tawi la Airport Bi.Hellen Mapunda.
Mhe.Raymond Mushi akiongea na sehemu ya wageni waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Tawi.
Mhe. Raymond Mushi akiwa kwenye picha ya pamoja na maofisa wa NMB mara baada ya uzinduzi
rasmi wa tawi la Gongo la Mboto.
SAFI SANA, TUNAOMBA NA KIMARA MWISHO MTUFUNGULIE TAWI, TUNAPATA SHIDA SANA MPAKA TUENDE MLIMANI CITY, JAMANI TUSAIDIENI. MKIFUNGUA KIMARA INA MAANA MBEZI, BONYOKWA, KING'ONGO, MATOSA, GOBA, MSUMI, MALAMBAMAWILI, KIBAMBA WOTE WATAPATA HUDUMA KIMARA, MAANA KITUO KIKUBWA KITAKUWA NI KIMARA MWISHO. TUSAIDIENI WADAU.
ReplyDelete