Na Andrew Chale

SAFARI Carnival kwa kushirikiana na Asia Idarous Khamsin (Fabak fashions) usiku wa 31/12/2014, Wameandaa shoo maalum ya Mkesha wa mwaka mpya 'Old Is Gold taarab', Ndani ya ukumbi wa Safari Carnival, Kawe jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin alieleza shoo hiyo maalum wadau

mbalimbali watakutana kuupokea mwaka kwa pamoja huku wakipata burudani ya muziki wa taarab wa zamani 'Old is Gold' pamoja na 'Surprise' kibao.

"Kwa kiingilio cha sh 5,000, tu, Fabaki fashions na Safari Carnival, tumeandaa usiku huu maalum wa Mkesha wa mwaka mpya.

Utakaoambatana na burudani ya taarab za zamani na za sasa pamoja na Surprise mbalimbali" alisema Asia Idarous.

Aidha,  Asia Idarous alisema usiku

huo, pia umedhaminiwa na Michuzi Media Group, Clouds fm,Gone Media, Maji Poa na wengineo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...