Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa Salome B. Misana (pichani) kuwa Mwenyekiti  mpya wa Bodi ya Baraza la Taifa la Hifadhi  na Usimamizi wa Mazingira ( NEMC).  Profesa Misana ni Mhadhiri Mwandamizi toka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam. Uteuzi huo umeanza rasmi tarehe 4/12/2014.

Wakati huo huo , Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira,  Dkt.  Binilith Mahenge amewateua Wajumbe  wa Bodi hiyo . 
Walioteuliwa ni Profesa Reuben Mwamakimbulah kutoka Chuo kikuu cha Sokoine Morogoro,  kitivo cha Misitu na Utunzaji wa mazingira, Injinia Bengiel  Humphrey Msofe ambaye ni  Mkurugenzi wa huduma za ufundi kutoka  Wizara ya Nishati na Madini , Bi Judica Haikase Kida Omari,  Kamishna Msaidizi  kutoka Wizara ya fedha na Uchumi.

Wajumbe wengine walioteuliwa ni Injinia Frida Rweyemamu, Mkuu wa Idara ya maji vijijini kutoka Wizara ya Maji, Ndugu Sheha Mjaja Juma   Mkurugenzi Idara ya Mazingira  kutoka Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Juma Mgoo ambaye  ni  Mkurugenzi  Mtendaji Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii , Bi Anna William Mtani, Mkurugenzi  Idara ya Maendeleo ya Miji  kutoka Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
 Mwingine ni Julius Keneth Ningu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais  yeye ni Mkurugenzi Idara ya Mazingira . Uteuzi huo unaanza rasmi tarehe  18/12/2014

      Imetolewa na
 KATIBU MKUU      
OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...