MFUKO wa Pensheni wa PSPF umedhamini mchezo wa kirafki
utakaowakutanisha wachezaji waliowahi kuwika katika timu kongwe nchini
Simba na Yanga.
Mchezo huo unatarajiwa kufanyika tarehe 1 Januari 2015 katika uwanja
wa chuo cha Bandari, Tandika jijini Dar es Salaam, kiingilio kitakuwa bure
ikiwa ni zawadi ya mwaka mpya kutoka PSPF.
Katika mchezo huo baadhi ya wachezaji wa Simba wanaotarajiwa kushuka
uwanjani ni Thomas Kipese, George Lucas, Bita John, George Masatu,
Mustafa Hoza, Emmanuel Gabriel, Idd seleman. Timu ya Simba inafanya
mazoezi katika uwanja wa Leaders uliopo Kinondoni, ipo chini kocha
mchezaji Kasongo Athuman.
Wanaotarajiwa kushuka uwanjani kwa upande wa Yanga ni Peter
Manyika, Mwanamtwa Kihwelo, Edibily Lunyamila, Mohamed Husein,
Chibe Chibindu, Aboukar Salum, Bakari malima. Yanga wanafanya
mazoezi katika uwanja wa kauda ulipo katika makao makuu ya klabu hiyo
kariakoo Jijini Dar es Salaam, wakiongozwa na kocha Peter Tino.
Lengo la mchezo huo ni kutoa burudani kwa wakazi wa Jiji la Dar es
Salaam na maeneo ya karibu hususani katika kipindi hiki cha sikukuu za
mwisho wa mwaka. PSPF itatumia fursa hiyo kutangaza huduma zake
mpya ambazo Mkopo wa Elimu na Mkopo wa Kuanza Maisha.
Tunatoa
mwito kwa wapenzi wa soka kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo ili
kuwaona wakongwe waliowahi kutikisha nchi katika anga ya soko nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...