.jpg)
Taarifa
iliyotolewa Desemba 11, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y.
Sefue inasema kuwa kabla ya uteuzi wake, Bwana Mafuru alikuwa Mkuu wa Idara ya
Rasilimali Fedha katika Ofisi ya Rais inayohusika na ufuatiliaji Miradi ya
Matokeo Makubwa Sasa (PDB). Aidha Bwana
Mafuru pia alikuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Benki ya FBME iliyowekwa chini ya
uangalizi wa muda wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Wakati huohuo,
Taarifa ya Balozi Sefue inasema Rais Kikwete amemteua Bibi Beng’i Mazana Issa
kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kuanzia
tarehe 4 Desemba, 2014. Kabla ya uteuzi
wake, Bibi Mazana Issa alikuwa Mkurugenzi wa Utawala wa Fedha katika Tume ya
Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS).
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa
Dominic M. Kambarage kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Kipya cha Kilimo cha
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuanzia tarehe 5 Desemba, 2014.
Taarifa
iliyotolewa Desemba 11, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue
imesema kabla ya kuteuliwa kwake kuwa Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Kambarage
alikuwa Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Sokoine, Morogoro.
Taarifa ya
Balozi Ombeni Sefue imesema kufuatia kuanzishwa kwa Chuo hicho kingine cha
Umma, Rais Kikwete pia amemteua Profesa Lesakit S. Mellau kuwa Naibu Makamu
Mkuu wa Chuo hicho upande wa Taaluma kuanzia tarehe 5 Desemba, 2014, na kabla
ya uteuzi wake, Profesa Mellau pia alikuwa Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha
Sokoine, Morogoro.
Aidha Taarifa ya
Balozi Sefue imesema Rais Kikwete amemteua Profesa Msafiri M. Jackson kuwa
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
(Utawala) kuanzia tarehe 5 Desemba, 2014.
Kabla ya uteuzi huo, Profesa Jackson alikuwa Mratibu wa Masomo ya
Taaluma za Shahada za Juu katika Chuo Kikuu cha Ardhi, Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bi.
Katarina Tengia Revocati kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani kuanzia tarehe 5
Desemba, 2014. Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa leo Desemba 11, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue,
imesema kabla ya uteuzi huo, Bi. Revocati alikuwa Msajili wa Mahakama Kuu,
Divisheni ya Biashara.
Vilevile katika
Taarifa hiyo, Rais Kikwete pia amemteua Bwana Rugalema J. Kahyoza kuwa Msajili
wa Mahakama Kuu kuanzia tarehe 5 Desemba, 2014.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Kahyoza alikuwa Hakimu Mwandamizi Msaidizi,
Mahakama Kuu, Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Menejimenti na
Mashauri.
Katika hatua
nyingine, Rais Kikwete amemteua Dkt. Fidelice Mafumiko kuwa Mkuu wa Taasisi ya
Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kuanzia tarehe 4 Desemba, 2014. Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Mafumiko alikuwa
Naibu Mkuu TEWW.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu
– Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...