DSC_0378
Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, James Kajugusi (mwenye suti nyeusi) aliyewamwakilisha Waziri mwenye dhamana wa wizara hiyo, akiongea na Vijana wanaofanyashughuli za kutolea wakati wa maadhimisho ya siku ya kujitolea kimataifa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.

Alisema ingawa kujitolea kunawezesha kupata uzoezi ili vijana waweze kuajiriwa na kuendeleza taaluma,maana ya kujitolea haipo katika kuajiriwa bali katika hali ya kuona maana yake katika kusaidia jamii kujitambua na kujituma na kuwajibika .
“Usaidizi katika jamii ndio muhimu kuliko ajira. Haina maana yoyote kuwa na ajira bila kujua maana yake katika kusaidiajamii,”  huku akisisitiza kwamba haina maana yoyote kama umeajiriwa na ukaendekeza umimi  huku ukiwa hujali maslahi ya umma hata yanapoharibika.
Alisema Serikali ikiwa inaamini kwamba chachu ya kujitolea  ni vijana ametaka watumie njia mbalimbali katika shughuli za kujitolea kwa kuona wenzetu wanafanya nini na kutumia uzoefu wao katika kujenga taifa imara la Tanzania.
Aidha alisema wakati umefika wa vijana kusaidia kurejesha moyo wa kujitolea uliokuwepo kabla ya miaka ya 1970 ambapo shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara ulifanywa na wananchi wenyewe kwa namna ya kujitolea kuanzia miaka ya 1970 moyo wa kujitolea umepungua sana.
DSC_0218
Pichani juu na chini ni baadhi ya vijana kutoka taasisi mbalimbali na mashirika yasiyo ya kiserikali waliohudhuria maadhimisho ya siku ya kujitolea kimataifa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma wakisikiliza kwa umakini hotuba ya Waziri Mukangara iliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, James Kajugusi (hayupo pichani).
“Nilikozaliwa wananchi ndio walikuwa wanatengeneza barabara, visima vya maji, wananchi ndio wanapeleka wagonjwa hospitali..’” na kusema kwamba sasa hali imekuwa mbaya kwa kuwa inadaiwa kitu kwanza kabla ya kufanyika kwa kazi.
Akizungumzia kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya kujitolea inayosema; Ushiriki na ushirikishwaji katika kuleta maendeleo katika ngazi zote za kitaifa na za kimataifa, amesema inaangalia  ushiriki wa vijana katika maendeleo.
Alisema Tanzania imetengeneza mikakati kadha aya kuwezesha ushiriki wa vijana ikiwa ni pamoja na kuridhia mkataba wa vijana wa umoja wa Mataifa na kuanzisha baraza la vijana kwa mujibu wa katiba.
Naye Afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo akizungumza kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodrigues, amesema umoja wa mataifa unajisikia faraja kuadhimisha siku hiyo ikiwakumbuka watu mbalimbali waliofanya utu kwa kujitolea katika shughuli mbalimbali za ubinadamu.
DSC_0223
Akiwasilisha neno la katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki moon alisema siku ya kimataifa ya kujitolea ni muhimu kutokana na mahitaji halisi yaliyopo sasa duniani katika ulinzi wa maisha ya binadamu na utamaduni wake.
Alisema maelfu ya wananchi waliokumbwa na madhila mbalimbali wameweza kutulizwa na wafanyakazi wa kujitolea ambao waliondoa umimi na ubinafsi na kusaidia walio katika matatizo.
Alisema Umoja wa mataifa ukiwa unathamini amani , haki sawa na maendeleo ya jamii na kwa kuwa na siku ya kujitolea ya kimataifa kunaonesha umuhimu wa juhudi za umoja huo za kusambaza malengo hayo kufanikisha maendeleo na ushiriki wa vijana katika maendeleo yao , kitaifa na kimataifa.
Katika hotuba yake ya kumkaribisha mgeni rasmi, Vuzo alisema kwamba shughuli za kujitolea za Umoja wa Mataifa zilianza nchini mwaka 1974 katika misingi ile ile ya kufunza jamii kujitolea kwa manufaa yao na maendeleo ya Taifa. Kwa habari na picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...