Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante
Olegabriel aliyesimama akifungua Mkutano Baadhi ya wasambazaji wa Filamu nchini (hawapo
pichani)kuhusu kuporomoka kwa bei ya filamu, wa pili kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa
Bodi ya Filamu nchini. Bi. Joyce Fissoo.Mkutano huo ulifanyika jana jijini Dar es Salaam
Na Genofeva Matemu – Maelezo
Serikali imewapongeza wasambazaji na wadau wa filamu nchini kwa mchango wao mkubwa
katika kuelimisha, kuhabarisha na kufundisha maadili ya mtanzania huku wakichangia katika
pato la taifa na kukuza uchumi wa nchi.
Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Profesa Elisante Ole Gabriel alipokua akifungua mkutano wa serikali na wasambazaji wa filamu
nchini jana jijini Dar es Salaam kujadili uporomokaji wa bidhaa za filamu nchini.
“Tunathamini sana kazi mnayoifanya, Serikali inawajali na ipo tayari kushirikiana nanyi kwa
kazi nzuri mnayoifanya hivyo ni vema kufanya mkutano huu kuwa wa kisanyansi kwa kuangalia
gharama mnazotumia kuandaa bidhaa za filamu ili kuweza kukua kibiashara na kukuza uchumi
wa nchi” amesema Pro. Gabriel.
Akizungumza wakati wa mkutano huo Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fisoo
amesema kuwa Bodi haitaruhusu bidhaa zilizo chini ya kiwango kupelekwa kwa watanzania kwa
daraja la bei ya chini pamoja na soko huria kwani hakuna uhuria usio na mipaka.
Bibi Fisoo amesema kuwa wananchi siyo dust bin wanapaswa kupelekewa kazi bora na zenye
hadhi kwani Bodi inahitaji kujiridhisha kuhusu viwango vya filamu hizo na kuheshimu fedha za
watanzania kwa kuwauzia kazi bora zinazoendana na thamani ya fedha zao.
Aidha Mwenyekiti wa wasambazaji wa bidhaa za filamu nchini Bw. Emmanuel Miamba
amewataka wadau na wasambazaji wa filamu nchini kuwa wakweli, wazalendo, pasipo kuogopa
kitu chochote na kuangalia maslai ya wasambazaji wote na kama wataona uwekezaji katika kazi
za filamu haulipi basi wawekeze katika masuala mengine na sio kushusha bei kuua tasnia ya
filamu nchini.
Naye Bw. Chacha Matula kutoka Jembe entertainment amewaomba wasambazaji kuwa na umoja
na mshikamano utakaowawezesha kushirikiana kwa pamoja na serikali kusitisha uporomokaji
wa bei za filamu na kuwadhibiti watu wanaotaka kuua kampuni za wasambazaji wadogo nchini.
Katika kuangalia quality ya filamu ni vyema kuacha kujifanya wazungu saaaana kupitiliza. Maoni yangu ni kama yafuatayo:
ReplyDelete1. Mavazi yanatakiwa yawe ya heshima ili kuendeleza utamaduni wetu.
2. Hakuna haja ya kuweka part 1 na 2, ni vyema filamu ikawa nzuri na ikafanyiwa editing ya kutosha. Parts 1 na 2 zinatuboa ijapokuwa wao wanaona ndiyo mpango wa kupatia fedha.
3. Scenes zinachukuwa muda mrefu sana mpaka zinachosha (mfano ngoma itachezwa weeeee mpaka unachoka kuangalia) ili kuvuta iwe na part nyengine (hii inahusiana na hapo juu).
4. Wacheza filamu na wanaofanya shughuli nyengine zinazohusiana na uzalishaji filamu waende shule wakajifunze ili kuboresha quality ya michezo yao.