Na Chalila Kibuda,
Globu ya Jamii, Dar es salaam
Globu ya Jamii, Dar es salaam
Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan mwinyi leo ameongoza mamia ya waombolezaji kwenye mazishi ya Sheikh Ali Mzee Comorian yaliyofanyika leo katika makaburi ya Wangazija yaliyopo katika barabara ya Bibi Titi Mohamed jijini Dar es Salaam.
Mazishi hayo pia yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim, Naibu Waziri wa Fedha, Mhe Adam Malima, Mufti Mkuu Sheikh Simba Shaban Bin Simba, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum na viongozi wengine.
Mazishi ya Sheikh Comorian yamefanyika huku mvua kubwa ikinyesha kwa takriban masaa mawili mfululizo.
Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiongea katika msikiti wa Makonge ilikofanyika swala ya mazishi alisema kifo cha sheikh huyo ni mipango ya Mungu na kwamba kila mtu safari yake ipo.

Alisema kifo cha sheikh kinatakiwa kuenziwa kwa mema aliyoyafanya katika uhai wake katika kupigania na kuendeleza Uislamu.
Rais Mstaafu wa awamu ya pilimAlhaj Ali Hassan Mwinyi (wa tatu kushoto),Waziri Mkuu Mstaafu,Dkt. Salim Ahmed Salim (wa nne kulia), Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Simba Shaaban Simba (wa pili kushoto) na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mussa Salum (wa tatu kulia) wakijumuika pamoja na waombolezaji wengine kwenye mazishi ya Sheikh Ali Mzee Comorian, katika makaburi ya Wangazija mtaa wa Bibi Titi Mohamed,jijini Dar es salaam mapema leo.
Picha na Othman Michuzi/Emmanuel Massaka.
Picha na Othman Michuzi/Emmanuel Massaka.
Sehemu ya Umati wa Waombelezaji ukiwa umebeba Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Sheikh Ali Mzee Comorian ukiwasili kwenye Makaburi ya Wangazija mtaa wa Bibi Titi Mohamed,jijini Dar es salaam huku mvua kubwa ikinyesha mapema leo.
Waombolezaji wakiendelea na shughuli ya Mazishi ya Marehemu Sheikh Ali Mzee Comorian kwenye Makaburi ya Wangazija mtaa wa Bibi Titi Mohamed, jijini Dar es salaam licha ya mvua kubwa kunyesha mapema leo.
sina uhakika wala simjui huyu nd ali mzee , ila kwa dalili inaonyesha alikuwa mtu mwema na mwadilifu , mpaka mawingu yamelia leo kwa kuleta mvua kali ktk majira haya ya joto , kwa kufariki kwa mja huyu wa mola mtukufu , mungu amrehemu.
ReplyDelete