Familia ya Captain Narcis Mapunda wa Mikocheni B (TPDC)
Dar es salaam, kwa masikitiko na huzuni wanatoa taaifa ya
msiba wa mtoto wao mpendwa;
ELIAS NARCIS MAPUNDA
Kifo hicho kilichotokea siku ya Ijumaa tarehe 28 November
2014 hapa jijini Dar es salaam.
Mipango ya mazishi
inafanyika nyumbani kwa Baba mzazi Captain Narcis
Mapunda, pale mikocheni, Nyumbu Street (pandisha mtaa
wa mikocheni Wariob tokea Mwai Kibaki Rd, baada ya Kanisa
la Mt Martha ingia mtaa unaofuata kulia).
Maandalizi ya awali yanalekea kuwa na ratiba ifuatayo ya
mazishi; mazishi yatafanyika kinondoni Makaburi ya Jumuiya
ya Madola (ndani ya ukuta) siku ya alhamisi tarehe 4
December 2014 majira ya saa 10 jioni (1600 hrs).
Awali ya
hapo kutakuwepo misa fupi, chakula pamoja na za heshima
za mwisho nyumbani kwa Capt Mapunda, ikifuatiwa na misa
maalum pale jirani kanisa la Mt Martha. Ratiba ya shughuli
zote inatarajiwa kuanza saa 4.30 asubuhi ya siku hiyo
(1000hrs).
Habari za msiba huu ziwafikie wana-Mapunda popote pale
walipo pamoja na nduguwote na marafiki.
Waweza kumpigia Mama Suzanne Mapunda kwa kujua taarifa
zaidi - 0754 884104.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...