SHIRIKA
LA USAFIRI DAR ES SALAAM (UDA)
SHIRIKA la Usafiri Dar es Salaam (UDA)
linawatangazia Watanzania wote hususan wakazi wa jiji la Dar es Salaam kwamba
linahitaji kuajiri madereva kwa ajili ya
kuendesha mabasi yake hapa jijini.
SIFA
ZA WAOMBAJI
Waombaji wa kazi ya udereva wanatakiwa kuwa na umri
wa kuanzia miaka 30-55, ujuzi wa udereva wa mabasi kutoka katika vyuo vya VETA,
NIT, au chuo kingine kinachotambulika na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi nchini
(NECTA). Pia wanapaswa kuwa na leseni ya udereva daraja C Kavu (Class C Plain)
na daraja C1(Class C1) , rekodi nzuri ya utendaji na afya njema.
NAMNA
YA KUOMBA
Waombaji wote walete barua zao za maombi
wakiambatanisha na barua za udhamini, walete barua hizo kwa mkono katika Ofisi
ya Afisa Rasilimali watu na Utawala, Makao Makuu ya UDA, KAMATA COMPLEX, mahali
zilipokuwa ofisi za mabasi ya SCANDINAVIA.
Wanawake wanyesifa wanahimizwa zaidi.
KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA NAMBA 255222127421,
0766777754, 0766777753 ,0754776700, 0715776500,0712000037 au wasiliana kwa
barua pepe info@uda.co.tz, uda@umojainvestments.com au kwa
sanduku la posta
Shirika la Usafiri Dar Es Salaam (UDA)
S.L.P 872
Dar Es Salaam,Tanzania
LIMETOLEWA
NA OFISI YA MAHUSIANO YA UMMA UDA
DESEMBA
01, 2014.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...