Mfuko wa Maendeleo ya jamii-TASAF kwa ushirikiano na
Wizara ya Fedha umempongeza na kumuaga rasmi Afisa aliyestaafu kutoka
Benki ya Dunia ofisi ya Tanzania ambaye alikuwa akisimamia shughuli za TASAF Bi. Ida Manjolo.
Bi. Manjolo ambaye amefanya kazi hapa nchini kwa miaka
kumi amepongezwa kwa kushiriki kikamilifu katika kuchochea kasi ya utekelezaji
wa shughuli za TASAF za kupambana na umaskini nchini .
Akizungumza katika hafla ya kumuaga na kumpongeza Afisa aliyestaafu kutoka
Benki ya Dunia ofisi ya Tanzania ambaye alikuwa akisimamia shughuli za TASAF (Task team Leader-TTL) Bi. Manjolo, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw.
Ladislaus Mwamanga alibainisha kuwa Afisa huyo alikuwa akitumia falsafa yenye
maneno ya "hakuna kulala hadi kieleweke" katika kuwapa moyo watendaji
na wadau wa mfuko huo katika kuwahudumia walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya
Maskini unaosimamiwa na TASAF.
"Wote tunafahamu kuwa katika kipindi ambacho
tumekuwa naye, TASAF sasa imepanda chati sana na siyo ndani ya nchi tu, lakini
pia hata nje ya nchi huko kwingineko Duniani, na maendeleo ya mpango wa
kunusuru Kaya Maskini umekuwa ukiongelewa kwamba ni mpango unaofanya vizuri,
lakini haya yote ni kwa sababu ya ushiriki wake mzuri ambao ulikuwepo na
amehusika kwa kiasi kikubwa kuuandaa na kuufikisha mahala hapa pazuri tulipo"
alifafanua Bw. Mwamanga.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha Dakta Servacius
Likwelile amemtaja Bi Manjolo kama kiongozi hodari ambaye wakati wote
amekuwa akitekeleza majukumu yake kwa ukamilifu na kuhakikisha kuwa mafanikio
yanapatikana.
"Tumekuwa katika safari ndefu lakini yenye
mafanikio makubwa kutokana na umakini wa mmoja wa madereva wetu ambaye ni Bi.
Manjolo , tulianza naye akiwa ni msaidizi wa TTL hadi akawa TTL na katika
kipindi chake chote cha miaka kumi ameiwezesha TASAF kufikia mahala hapa kwa
sababu ya uwazi , wepesi na ukarimu wake wa kutaka kuona kwamba
tunafanikiwa". Alibainisha Dr. Likwelile.
Dr. Likwelile ambaye
pia amepata kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha hakusita kutoa shukrani zake za dhati kwa mafanikio
yaliyopatikana kutokana na ushiriki wa Bi. Manjolo.
"Tunamshukuru Aida kwa uadilifu, uaminifu, ukaribu,
udugu na kupenda kutimiza wajibu na akaongeza kuwa siyo rahisi kutekeleza
mpango kama huu na ukaleta maana kwa jamii kama hakuna uongozi mzuri na mshauri
mzuri". alisisitiza Dr. Likwelile. .png)
.png)
Afisa aliyestaafu wa Benki ya
Dunia aliyekuwa akisimamia shughuli za TASAF Bi. Ida Manjolo akifurahia tuzo
aliyopewa na TASAF kama ishara ya mafanikio makubwa kufuatia ushirikiano
alioutoa kwa TASAF katika kutekeleza mipango ya maendeleo.
Menejimenti ya TASAF ikiwa katika picha ya pamoja na Afisa aliyestaafu wa
Benki ya Dunia aliyekuwa akisimamia shughuli za TASAF Bi. Ida Manjolo (wa
tatu toka kulia walioketi).
Baadhi ya wafanyakazi wa TASAF wakiwa katika picha ya
pamoja na Afisa aliyestaafu wa Benki ya Dunia aliyekuwa akisimamia
shughuli za TASAF Bi. Ida Manjolo (wa tatu toka kulia walioketi) wakati wa
hafla ya kumuaga Bi. Manjolo. .png)
.png)
Afisa aliyestaafu wa Benki ya Dunia aliyekuwa
akisimamia shughuli za TASAF Bi. Ida Manjolo (wa tatu toka kulia walioketi) akiwa
katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dokta Servacius
Likwelile, Kamishna wa Fedha za nje Wizara ya Fedha Bw. Said
Magonya (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga
(wa kwanza kushoto). Wengine ni walioketi toka kulia ni Afisa mpya wa
Benki ya Dunia anayesimamia shughuli za TASAF Bw. Mohamed Muuderis na Naibu Katibu
Mkuu ofisi ya Rais Ikulu Bi. Suzan Mlawi pamoja na baadhi ya wanafamilia ya Bi
Manjolo (waliyosimama).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...