Rais Wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Mh Jamal Malinzi akizungumza na wanahabari leo katika ofisi za TFF kuhusu kampuni ya Proin Promotions ltd kudhamini Mashindano ya mpira wa miguu kwa wanawake yajulikanayo kama Kombe la Wanawake Taifa, mashindano hayo yanatarajiwa kuanza tarehe 28 Disemba kwa kushirikisha timu kutoka Mikoa yote ya Tanzania. Mashindano hayo yatazinduliwa Mkoani Mwanza kwa kuzikutanisha timu za Mwanza na Mara. Kushoto kwa rais wa TFF ni Rose Kissiwa ambae ni mwakilishi wa Chama cha Mpira wa wanawake Tanzania.Na Kulia ni Mkurugenzi wa Makampuni ya Proin , Johnson Lukaza ambao ndio wadhamini wakuu wa Kombe la Wanawake Tanzania.
 Mkurugenzi wa Makampuni ya Proin , Johnson Lukaza akizungumzia jinsi kampuni ya Proin Promotions Ltd ilivyoona umuhimu wa kuchangia katika kuinua soka la wanawake nchini na kuamua kudhamini Shindano hilo lijulikanalo kama Kombe la Wanawake Taifa ambalo litaanza rasmi tarehe 28 kwa mechi ya uzinduzi kati ya Mwanza na Mara huko Mkoani Mwanza
Bi Rose Kissiwa, Mwakilishi wa Chama cha Mpira wa Wanawake Tanzania akizungumzia juu ya udhamini uliotolewa na kampuni ya Proin Promotions Ltd katika kufanikisha Mashindano ya Mpira wa miguu kwa Wanawake yajulikanayo kama Kombe la Wanawake Taifa ambapo uzinduzi wa Mashindano hayo yatafanyika Jijini Mwanza kwa kuzikutanisha TImu za Mwanza na Mara.Picha zote na Josephat Lukaza. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...