SAM_0035
Wachezaji wa Timu ya EALA waliovalia jezi rangi ya blue wakipambana na wenzao timu ya Burundi.
 
Timu ya wabunge wa EALA wameicharaza mabao manne kwa mbili timu ya Burundi jana katika Uwanja Sheikh Amri Abeid  jijini Arusha ikiwa ni muendelezo wa mashindano ya wabunge Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
Mchezaji mahiri wa timu ya Eala John King aliipatia mabao 3 timu yake dakika ya 9 na 21 kipindi cha kwanza hali iliyosabaisha mashabiki waliomiminika katika uwanja huo kumshangila
Kipindi cha pili hali ilibadilika  baada ya timu ya Burundi kujipatia mabao mawili  dakika ya nne na dakika ya 18, mpigaji wa magoli hayo ni Simon Gahinja

Baada ya mchuano mkali wa timu zote mbili ,Eala waliongeza bao la 4 lililofungwa na mchezaji Wilyclif Keto dakika ya 25 baada ya kupata penalt dakika 33  ambapo mpigaji penalt alikosa baada ya mlinda mlango wa Burundi Ibrahim Uwizey kudaka
SAM_0039Mbunge wa EALA kutoka nchini Tanzania Mh.Twaha Taslama jezi namba 12 akiwa uwanjani
SAM_0038Mh Mbunge wa Eala Bernad Mrunya akiwa anajiandaa kukabilia na timu ya Burundi katika Uwanja Sheikh Amri Abeid  jijini Arusha ikiwa ni muendelezo wa mashindano ya wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).(Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog Arusha)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...