Na Sultani Kipingo
Taasisi za serikali, mashirika ya umma wizara na idara mbalimbali za serikali zimeshauriwa kushiriki katika mashindano ya uwasilishaji wa taarifa bora za fedha za mwaka tofauti na ilivyo sasa ambapo makundi haya yamekuwa yakishiriki kwa uchache sana na sehemu kubwa ya washiriki kuachiwa taasisi na mashirika binafsi.
Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji tuzo na vyeti kwa washindi katika uwasilishaji wa taarifa bora za fedha mwaka 2014, Naibu Waziri wa Fedha, Mhe Adamu Malima amesema ni wakati mwafaka kwa taasisi na idara mbalimbali za serikali kuingia katika mashindano hayo ili kujipima na kuongeza ufanisi katika utunzaji na uandaaji wa taarifa zao kulingana na viwango vya kimataifa IFRS.
Katika mshindano hayo ambayo huratibiwa na bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu nchini NBAA kwa mwaka huu jumla ya washiriki 40 walishiriki ambapo mamlaka ya mapato nchini TRA Iliibuka mshindi wa kwanza kwa uwasilishaji wa taarifa bora za fedha kwa mwaka 2013 -2014. kwa upande wa taasisi za serikali.
Kamishna Mkuu wa TRA Rished Bade akizungumza na waandishi wa habari mara
baada ya kupokea tuzo za kuweka mahesabu vizuri kwa taasisi bora za
serikali mwaka 2013-2014 iliyotolewa NBAA.
Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima (kushoto) akimkabidhi
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Rished Bade Ngao ya ushindi wa kwanza
kwa taasisi za serikali kwa kuweka kumbukumbu za mahesabu vizuri mwaka
2013/14 inayotambuliwa na Bodi ya Wakaguzi wa Mahesabu nchini (NBAA), juzi
mkoani Arusha, wanaoshudia ni wafanyakazi wa TRA.
Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima akifurahia jambo na Kamishna Mkuu wa TRA Rished Bade.
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi pamoja na viongozi na watumishi wa TRA.
Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima akifurahia jambo na Kamishna Mkuu wa TRA Rished Bade.
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi pamoja na viongozi na watumishi wa TRA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...