Na. Mwandishi Wetu
Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Operesheni Tokomeza
itakusanya taarifa na kupokea malalamiko yaliyotokana
na utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili Nchini
mikoa ya Mikoa ya Arusha, Manyara, Tabora, Singida na
Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa tarehe 24 Desemba,
2014 na Katibu wa Tume hiyo, Bw.Frederick Manyanda,
Tume inatarajiwa kuendelea na zoezi la kukusanya maoni
na taarifa kuanzia tarehe 5 Januari , 2015 mpaka tarehe
21 Januari,2015 katika maeneo mbalimbali ya kanda ya
Kaskazini na Kati Nchini.
Katika kutekeleza jukumu hilo, Bw. Manyanda ameeleza
kuwa, Tume itatembelea Mkoa wa Tabora tarehe 4 Januari
2015 mpaka tarehe 8 Januari 2015 na itakuwa Mkoa
wa Singida tarehe 9 Januari,2015 mpaka tarehe 10
Januari,2015.
Aidha Tume itatembelea Mkoa wa Dodoma tarehe 11
Januari, 2015 mpaka tarehe 12 Januari 2015. Vilevile,
Wakili Manyanda ameeleza kuwa Tume itakusanya maoni
Mkoa wa Manyara kuanzia tarehe 13 Januari, 2015 mpaka
tarehe 16 Januari, 2015 na Tume itakuwa Mkoa wa Arusha
tarehe 16 Januari 2015 mpaka tarehe 19 Januari,2015.
Mpaka sasa Tume ya Rais ya Operesheni Tokomeza
imefanikiwa kukusanya taarifa na kupokea malamiko
yaliyotokana na utekelezaji wa Operesheni Tokomeza
katika mikoa kumi na tano (15) ya Tanzania Bara
ambayo ni Kigoma, Katavi, Rukwa, Mbeya Kagera,
Geita, Shinyanga, Simiyu, Mwanza
Mara,Lindi,Mtwara,Ruvuma,Iringa, Morogoro.
Pamoja na mikutano hiyo, Bw. Manyanda ametumia fursa
hiyo kuwakumbusha na kuwaomba wananchi na watanzania
wa maeneo husika kuendelea kutuma taarifa na
malalamiko kuhusu utekelezaji wa Operesheni Tokomeza
kwa njia ya barua, simu na barua pepe ambapo ameeleza
kuwa wananchi wanaweza kutuma barua kwa Katibu wa
Tume, Tume ya Uchunguzi wa Operesheni Tokomeza
Ujangili, SLP 9050, Dar es Salaam na barua pepe kwenda
opereshenitokomeza@agctz.go.tz.Aidha, wananchi wa
maeneo husika wanaweza kutuma ujumbe mfupi wa
maandishi kwa namba za simu za Tigo: 0714 826826;
Vodacom: 0767 826826; Airtel: 0787 826826; na Zantel:
0773 826826.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...