Mratibu
wa Uhurumarathon Tanzania Innocent Melleck akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar Es Salaam juu ya kukamilika kwa maandalizi yam bio
hizo zinazotarajiwa kufanyika jumapili hii jijini Dar Es Salaam katika
viwanja vya Leders Club kushoto ni katibu mkuu wa shirikisho la Riadha
la Taifa Selemani Nyambui.
MAANDALIZI ya mbio za Uhuru, Uhuru Marathon, zinazotarajiwa kufanyika Desemba 7 (jumapili)
jijini Dar es Salaam yamekamilika, huku wanaridha kadhaa kutoka ndani na
nje ya nchi wakithibitisha kushiriki mbio hizo zenye lengo la kuulinda
uhuru wetu, kudumisha umoja, amani, upendo na mshikamano miongoni mwa
Watanzania.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Mratibu wa Uhuru Marathon, Innocent
Melleck alisema, maandalizi yote yamekamilika, huku wanariadha wa hapa
nchini kutoka nje ya Dar es Salaam wakiwa wamewasili tayari kwa ushiriki
wao.
Melleck
pia alisema, kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi ulinzi umeimarishwa
kwa kiwango kikubwa ili kuhakikisha usalama unakuwa mkubwa kwa washiriki
wote na barabara zitakazotumika zitafungwa katika kipindi hicho.
“Kila
kitu kimekamilika na washiriki kutoka nje ya Dar es Salaam wameanza
kuwasili kwa ajili ya mbio hizo na tunawahakikishia usalama utakuwa
mkubwa mno katika kipindi chote cha mbio hizo n mpaka kufikia jana
(juzi) tayari washiriki waliojitokeza walikuwa 4000,” alisema.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Selemani Nyambui alisema,
wanariadha maarufu wa hapa nchini watakaoshiriki ni pamoja na Fabian
Joseph na Dickson Marwa, huku Jacqueline Sekini aliyeshinda mbio hizo
kwa upande wa wanawake mwaka jana, naye akiapa kutetea ubingwa wake.
“Wapo
wanariadha wengi watakaoshiriki, lakini nataka kutoa angalizo kwa
wanariadha kutoka Kenya, sisi tumetumwa mwaliko kwa wa chama husika na
wao ndio watutumia majina ya wanariadha kumi, watano wa kiume na
waliobaki wa kike, hatutapokea mwanariadha kutoka nchi hiyo ambaye
hatujapewa jina lake,” alisema.
Nyambui
alisema, tayari waamuzi watakaosimamia mbio hizo wapo tayari na
akasisitiza ni lazima taratatibu zote zitafuatwa ili kupata mshindi
halali.
Mbio
hizo zinatarajiwa kuanzia viwanja vya Leaders Club na zitakuwa za
kilomita 21, kilomita 5 na kilomita 3 ambazo ni maalumu kwa ajili ya
viongozi wa kitaifa, dini na taasisi mbalimbali.
Aidha Melleck alisema, tayari namba kwa washiriki zimeanza kutolewa na wanaweza kuzipata katika viwanja vya Leaders Club.
Mgeni rasmi katika mbio hizo anatarajiwa kuwa Rais Jakaya Kikwete.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...