Ujumbe wa wataalamu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania ( TPA) unatembelea
Bandari ya Singapore (PSA) ili kubadilishana utaalamu wa namna ha
kuongeza ufanisi na kuimarisha Ulinzi na usalama wa Bandari kwa kutumia
Mitambo ya kisasa na Teknolojia ya Habari na mawasiliano (ICT) , Ujumbe
wa TPA unaongozwa na Ndg. Phares Magesa , Mkurugenzi wa ICT wa TPA, pia
wamo wahandisi wa majengo, wataalamu wa Ulinzi na wataalamu wa TEHAMA.
Ziara hii ni muendelezo wa ushirikiano wa PSA na TPA ikiwa ni sehemu ya
makubaliano yaliyotiwa sahihi kati ya TPA na PSA wakati wa ziara ya Mhe.
Rais Kikwete alipotembelea nchini Singapore mwaka jana.
Ujumbe wa TPA ulipotembelea eneo la Bandari ya Singapore linalotumika
kwa ajili ya Meli za abiria, starehe na kuvinjari ( waterfront
development ).
Ujumbe wa TPA ukiwa kwenye chakula Cha pamoja na Ujumbe PSA
Ujumbe wa TPA ukiwa kwenye mazungumzo na Ujumbe wa PSA makao makuu ya PSA
Mkuu wa msafara Ndg. Magesa akisalimiana na Makamu wa Rais Msaidizi wa
PSA anayeshugulikia ICT Ndg. Andrew Gill wakati akiwakaribisha makao
makuu wa PSA
Mkuu wa msafira wa TPA Ndg. Magesa akipokea zawadi toka Makamu wa Rais
Msaidizi wa Mamlaka ya Bandari ya Singapore ( PSA) anayeshugulikia
biashara Ndg. Vignes kulia
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...