NA ANDREW CHALE
USIKU wa ‘Old Is Gold’ na Spice Modern Taarab, unatarajiwa kurindima kwa kishindo Jumapili ya kesho Desemba 7, ndani ya   ukumbi wa Thai Village  uliopo Masaki, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin, mwandaaji na mdhamini wa onyesho hilo, mashabiki  wa Old Is Gold  watakuwa wakikutana katika kiota hicho kipya cha burudani kila jumapili kukumbushana enzi.
“Kwa kiingilio cha sh 5,000 tu, wadau watafurahia shoo kabambe kutoka kwa Spice Modern Taarab ndani ukumbi wa Thai Village. Huku wadau wkijumuika pamoja na kubadilishna mawazo” alisema Asia Idarous.
Asia Idarous alilielezea kundi hilo ni la magwiji wa muziki huo wa mwambao ikiwemo kupiga nyimbo za taarab za zamani na zile za sasa ambapo miongoni mwa nyimbo  hizo ni pamoja na ‘Pendo kitu cha hiari’, ‘Dunia ina fisadi,’ ‘Kasha’ na nyingine nyingi.
Onyesho  hilo litakuwa kila siku kwenye ukumbi huo wa Thai Village huku likidhaminiwa na Fabak Fashions (Mikocheni) pamoja na Thai Village huku wadau wengine wakiwa ni pamoja na Clouds tv, Michuzi Media Group, G, One Media wengine wengi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...