Na Andrew Chale 
USIKU wa ‘Old Is Gold’ na Spice Modern Taarab, unatarajiwa kurindima  usiku wa Desemba 28, Mwaka huu ndani ya   ukumbi wa Safari Carnival uliopo Mikocheni B, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin, mwandaaji na mdhamini wa onyesho hilo,  mashabiki  wa Old Is Gold watapata burudani ya aina yake katika kiota hicho cha burudani kila jumapili kukumbushana enzi.
“Kwa kiingilio cha sh 5,000 tu, wadau watafurahia shoo kabambe kutoka kwa Spice Modern Taarab ndani ukumbi wa Safari Carnival. Huku wadau wakijumuika pamoja na kubadilishna mawazo” alisema Asia Idarous.
Asia Idarous alilielezea kundi hilo ni la magwiji wa muziki huo wa mwambao ikiwemo kupiga nyimbo za taarab za zamani na zile za sasa.
Onyesho  ni la kila siku za Jumapili kwenye ukumbi huo huku likidhaminiwa na Fabak Fashions (Mikocheni), Safari Carnival,  wadau wengine wakiwa ni pamoja na Clouds tv, Michuzi Media Group  na wengine wengi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...