Bodi ya Utalii
Tanzania (TTB) imeshirikiana na Timu
ya mpira wa miguu ya Sunderland ya Uingereza katika uzinduzi wa
utangazaji utalii wa Tanzania pamoja na uhamasishaji wa uwekezaji na maendeleo
ya michezo (Destination Partner in Tourism and Sports Development).
Uzinduzi
huo ulifanyika tarehe 29 Novemba, 2014 kwenye kiwanja cha “Stadium of Light”, kinachomilikiwa
na Sunderland Association Football Club (SAFC).
Tukio hilo lilihudhuriwa
na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Balozi Peter Kallaghe, Maafisa wa
Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza, Watanzania waishio nchini Uingereza
pamoja na baadhi ya maafisa wa Bodi ya Utalii Tanzania.
Wakati wa uzinduzi
huo katika kingo za kuta za uwanja yalionekana matangazo yanayotangaza vivutio
vya utalii vya Tanzania ambapo kulikuwa na mechi kati ya timu ya Sunderland na
Chelsea FC iliyorushwa moja kwa moja na kituo kinachorusha mechi mbalimbali za
mpira wa miguu cha DSTV. Aidha wachezaji wa timu ya Sunderland walionekana
wakiwa wamevaa jezi maalum zilizoandikwa
‘Visit Tanzania’ wakati wakifanya mazoezi kabla ya mechi hiyo.
Bodi ya Utalii
Tanzania imetumia fursa ya mechi hiyo kuhamasisha wageni mashuhuri kutoka ndani
na nje ya Uingereza pamoja na mashabiki wa Timu hizo wa nchi zote duniani
kutembelea vivutio vya utalii wa Tanzania.
Imetolewa na
BODI YA
UTALII TANZANI
01/12/2014
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...