DSC_0908
Mratibu wa Mradi wa Ukimwi ILO, Getrude Sima (kushoto) akitoa maelezo ya kikundi cha kina mama ambao ni walengwa wa mradi wa Ukimwi unaofadhiliwa na SIDA chini ya shirika la kazi duniani (ILO), kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, katika ziara ya kikazi ya kutembelea miradi inayosaidiwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani Iringa na Njombe. Kulia ni Practice Specialist HIV/AIDS, Dr Bwijo Bwijo.

Na Mwandishi wetu, Iringa.

KIKUNDI cha wafinyanzi wanawake cha Lungemba,kilichopo Wilaya ya Iringa, wameomba kusaidiwa vifaa vya kisasa vya ufinyanzi, ili waweze kutengeneza vitu bora vitakavyokubalika katika soko. Maombi hayo wameyatoa katika risala yao kwa Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Alvaro Rodriguez.

Mratibu huyo alikuwa katika ziara ya kikazi ya kutembelea miradi inayosaidiwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani Iringa na Njombe. Makundi yaliyotembelea ni yale ya ujasiriamali, yanayosimamiwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) chini ya mpango wa Kupunguza Maambukizi ya UKIMWI kwa Njia ya Uwezeshaji wa Kiuchumi kwa Wafanyakazi walio katika Sekta Isiyo Rasmi kando kando mwa Barabara Kuu iendayo Tanzania-Zambia maarufu kama “Corridor Economic Empowerment Project (CEEP) “

Aidha makundi mengine yaliyotembelewa ni ya wakulima wanaosaidiwa pembejeo na wanaotengeneza vikapu na kufanya shughuli binafsi ikiwamo mabucha. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...