Na Bakari Issa,Dar es Salaaam
Wajasiriamali
toka vikundi mbalimbali wamehamasishwa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya (NHIF) ili kurahisisha matibabu wawapo katika shughuli zao
za kawaida,leo katika ukumbi wa Msimbazi Centre jijini Dar es Salaam.
Katika
Mpango mpya uliozinduliwa na Mfuko huo ujulikanao kama Mpango wa
Kikoa(MATUAL PLAN),Wajasiriamali watakaojiunga na mfuko huo na kuwa
wanachama watalipia shilingi 76,800 kwa mwaka ili kupata matibabu
kupitia mfuko huo.
Akizungumza
na wajasiriamali kutoka vikundi mbalimbali ambavyo vipo chini ya
Muungano wa vikundi mbalimbali vya kuinua jamii(ASE),Mkurugenzi wa Mfuko
wa Afya ya Jamii kutoka Mfuko wa Bima ya Afya,Rehani Athumani amewataka
wajasiliamali wanaofanya biashara ndogondogo wasione ngumu kujiunga na
Mfuko huo wa Bima ya Afya na amewataka viongozi kuwa na ushirikiano
wanapopata matatizo na changamoto katika kufanikisha suala hilo.
“Wajasiriamali
wa biashara ndogondogo nawashauru kujiunga na mfuko huu,na nawasihi
viongozi wenzangu kuwa na ushirikiano tunapopatwa na matatizo pamoja na
changamoto”,alisema Rehani.
Kwa
upande wake,Afisa Matekelezo na Uratibu(NHIF),Catherine Masingisa
amesema kuwa mpango huo ni kwa wote,watoto na wakubwa kwa mjasiriamali
kuchangia mfuko huo wa Bima ya Afya,hata hivyo amesema mpango huo
utakuwa na matibabu sawa na ule mpango wa Watumishi wa Serikali.
“Mpango
huu wa Kikoa ni utaratibu wa kupata huduma ya afya kwa wajasiriamali
wadogowadogo katika vikundi na wanachama watapata huduma ya matibabu kwa
unafuu zaidi na kuondoa kabisa suala la unyanyasaji kwa
wajasiriamali”,alisema Catherine.
Naye,Mratibu
Mkuu wa ASE,Bi.Sunayritha Mapunda amewataka wajasiriamali hao walioko
katika muungano huo wa vikundi mbalimbali vya kuinua jamii kuonyesha
mfano kwa wajasiriamali wengine walioko nchini kujiunga na Mfuko huo wa
Taifa wa Bima ya Afya.
Mkurugenzi
wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Rehani Athumani akiongea na vikundi
mbalimabli vya wajasiliamali kuhusu umuhimu wa mfuko wa Afya ya jamii
pamoja na kuwahamasisha wajasiliamali hao kufungua bima ya afya kwa
ajili ya matibabu.
Mratibu
wa Mtandao wa Mfuko wa Afya ya Jamii(TNCHF), Camillius Mathew Haule
akitoa maelekezo juu ya ujazaji wa fomu za Mfuko wa Afya ya Jamii kwa
wajasiliamali hao
Afisa
Matekelezo na Uratibu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)
Catherine Masingisa akizungumza na wajasiliamali juu ya mfuko wa afya
unavyofanya kazi hapa nchini.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...