Imeelezwa
kuwa, wakaguzi wa migodi wanao mchango mkubwa katika kuepusha ajali zinazotokea
migodini hususani kwa wachimbaji wadogo endapo watatoa mapendekezo na maoni
yatakayowezesha kuandaa miongozo (checklist) itakayotumika katika ukaguzi wa
migodi.
Hayo
yameelezewa na Mtaalamu kutoka Idara ya Madini, Wizara ya Nishati na Madini ,
Mhandisi Noel Baraka wakati akitoa mada katika kikao kazi cha wakaguzi wa
migodi wanaokutana kwa lengo la kuandaa checklist zitakazotumika kwa ajili ya
shughuli za ukaguzi wa migodi.
Akizungumzia
hali halisi ya watalaamu hao, alieleza kuwa, bado kuna upungufu wa wakaguzi wa
migodi huku idadi kubwa ikiwa ni
watalaamu wachanga ambao bado hawana uzoefu wa kutosha katika shughuli hizo. “Pamoja
na upungufu huu lakini endapo tutaandaa checklist nzuri itasaidia kwa kiasi
kikubwa kuepusha ajali migodini,” ,alisisitiza Baraka.
Wakati
huo huo, akitoa mada katika kikao hicho, Mhandisi Assa Mwakilembe amewataka
wakaguzi hao kuzingatia maeneo muhimu mbalimbali ambayo yameainishwa katika Sheria ya Madini ya mwaka 2010
yakiwemo masuala ya uhifadhi wa mazingira, usalama na afya na kuwataka
wataalamu hao kutoa kipaumbele katika maeneo hayo wakati wa shughuli za ukaguzi
wa migodi nchini.
Vilevile,
akitoa mada ya namna ya kuandaa miongozo ya ukaguzi (checklist), Kamishna
Msaidizi anayeshughulikia Ukaguzi wa Migodi Mhandisi Ally Samaje ameeeleza
umuhimu wa kuwa na checklist katika shughuli za migodi kwamba, zitawezesha
kufahamu mapungufu yaliyoko migodini na hivyo kujua namna bora ya kutoa ushauri
wafanyapo ukaguzi katika migodi ya wachimbaji wakubwa na wadogo.
Washiriki wa kikao kazi cha kuandaa miongozo (checklist) ya ukaguzi wa migodi wakiwa katika makundi kujadiliana namna ya kuandaa miongozo hiyo.
Baadhi ya Wakaguzi wa migodi wakiwa katika majadiliano kuandaa checklist ya ukaguzi wa migodi.
Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha kuandaa checklist ya wakaguzi wa migodi wakiwa katika kazi za vikundi kuandaa miongozo hiyo.
Mratibu wa kikao kazi cha kuandaa checklist ya ukaguzi wa migodi, Mhandisi Assa Mwakilembe akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi cha kuandaa cchecklist ya ukaguzi wa mgodi.
Mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Idara ya Madini, Mhandisi Noel Baraka akiongea jambo wakati akitoa mada kuhusu Ukaguzi wa Madini wakati wa kikao kazi cha Wakaguzi wa Migodi nchini.Na Asteria Muhozya, Mwanza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...