Viongozi wa NATATA, toka kushoto ni Katibu Mkuu Halima Guga,Mwenyekiti Given Massawe na mratibu wa Elimu Abdulkarim Baksh.
Mwenyekiti wa NATASA ,Given Massawe akipozi kwa picha na
wadau wa NATASA, toka kushoto ni Henry Mzava,Evance,Letitia Smith
ambae yeye anatoka Namibia, Henry,Hamza Riyani, Charles na Mercy.
M/kiti wa NATASA Given
Massawe akikata keki ya ya kuzindua umoja huo pamoja kuazimisha miaka 53
ya Uhuru wa Tz huku katibu wake Halima Guga akishuhudia.
Wakina dada wa
Kitanzania wanaosoma kwenye mjii wa Nanchang ambao ni wanachama wa
NATASA wakipozi kwa picha wakiwa na bendera zao za Tanzania siku ya
uzinduzi huo.
.Wakina
dada wa Kitanzania wanaosoma kwenye mjii wa Nanchang ambao ni wanachama
wa NATASA wakipozi kwa picha wakiwa na bendera zao za Tanzania siku ya
uzinduzi huo.
wadau wa NATASA wakiwa ndani ya ukumbi wa Hotel ya XIN DIAN TI
wakibadilisha mawazo mawili matatu na kukumbushana story mbali mbali za
nyumbani Tanzania.
Mzee wa Shekeli Geofrey Njalangi na kitamba chake cheupe mkononi mbele
kabisa akisataka rhumba siku ya uzinduzi huo wa NATASA pamoja na Charles
kulia na Elvis kushoto kwake ndani ya ukumbi wa XIN DIAN TI HOTEL
kwenye mjii wa Nanchang nchini CHINA.
Mo van der
Mhando,Nanchang,
China.
Wanafunzi wa
Kitanzania wanaosoma kwenye mjii wa
Nanchang nchini China wameanzisha umoja wao na Jumamosi iliyopita wameuzindua rasmi umoja huo
wenye lengo la kuwasaidia kwa mambo mbali mbali wakiwa kwenye nchi ya kigeni.
Jumla ya
wanafunzi 54 wa Kitanzania wapo kwenye mjii huo wakiwa wanasoma kwenye vyuo
mbali mbali na walikuwa hawana kitu chochote kinachowaweka karibu kama
Watanzania na ndio maana wakaanzisha umoja huo.
Umoja huo
unaojulikana kwa jina la Nanchang, Tanzanian Students Association (NATASA)
ulizinduliwa rasmi na mwenyekiti wake Given Massawe ambae alisema kuanzishwa
kwa umoja huo lilikuwa ni wazo la muda mrefu na hatimae hivi sasa ndoto
imetimia.Massawe
alifafanua kuwa kwenye mingine ya nchini China ambako kuna wanafunzi wa
Kitanzania nao wanajumuia zao ambazo zinawasaidia hivyo kwa wanafunzi wa
Nanchang kuwa na umoja huo ni sehemu ya fungua milango kwao.
Mwenyekiti
huyo amesema hivi sasa wapo kwenye harakati za kutengeneza katiba yao ambayo ndio
itakuwa dira ya uongozi wao na pia kuzinduliwa kwa chama hicho ni msaada tosha kwa
wanafunzi hao wa Kitanzania kuanzia kwenye masomo hadi maisha ya kila siku.
Uzinduzi wa
umoja huo ulienda sambamba za sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania bara na
hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa wanafunzi wa Nanchang kusherekea siku yao ya
Uhuru wakiwa pamoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...