Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe
akifungua zoezi la uchangiaji wa harambee ya kupatikana kwa shilingi milioni 100 kwa ajili ya ununuzi
wa gari la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Jimbo la Kaskazini-Magharibi linalojumlisha
Wilaya ya Nachingwea, Ruangwa na Liwale mkoani Lindi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea,
Regina Chonjo, anayefuata ni Katibu Mkuu wa KKKT, Dayosisi ya Kusini –Mashariki, Jane Mkimbo.
Kulia ni Mkuu wa Jimbo hilo, Mchungaji Charles Mtweve. Katika harambee hiyo Shilingi Milioni 22.3
zilipatikana.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe
akitoa mchango wake wa awali shilingi milioni moja kwa ajili ya uchangiaji wa harambee ya kupatikana
kwa shilingi milioni 100 kwa ajili ya ununuzi wa gari la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),
Jimbo la Kaskazini-Magharibi linalojumlisha Wilaya ya Nachingwea, Ruangwa na Liwale mkoani Lindi.
Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo, anayefuata ni Katibu Mkuu wa KKKT,
Dayosisi ya Kusini –Mashariki, Jane Mkimbo. Wapili kulia ni Mkuu wa Jimbo hilo, Mchungaji Charles
Mtweve. Katika harambee hiyo Shilingi Milioni 22.3 zilipatikana.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe
(watatu kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo (wanne kushoto) wakiwa kwenye
picha ya pamoja na viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Jimbo la Kaskazini-
Magharibi, Nachingwea na KKKT Dayosisi ya Kusini-Mashariki, Kanisa Katoliki na maofisa wa wilaya
hiyo, mara baada ya kumaliza harambee ya kuchangisha milioni 100 kwa ajili ya ununuzi wa gari la
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Jimbo la Kaskazini-Magharibi linalojumlisha Wilaya ya
Nachingwea, Ruangwa na Liwale mkoani Lindi. Picha zote na Felix Mwagara
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...