Mshambuliaji wa Yanga,Hamis Tambwe akiipatia timu yake bao la kusawazisha katika mtanange wa muendelezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam leo.Mechi hiyo imemalizika kwa timu zote kufungana bao 2-2.Magoli ya Azam yametiwa kimiani na Didier Kavumbagu (dakika ya 5) na John Bocco (dakika ya 65) wakati magoli ya Yanga yakifungwa na Hamis Tambwe (dakika ya 7) huku goli la pili likufungwa na Simon Msuva (dakika ya 51).Picha zote na Othman Michuzi.
Mfungaji wa goli la kwanza kwa timu ya Yanga,Hamis Tambwe na Mfungaji wa Bao la pili,Simon Msuva wakishangia ushindi wao dhidi ya timu ya Azam katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam leo.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia ushindi na Washabiki wao.
Wachezaji wa timu ya Azam FC wakishangilia goli yao la kwanza dhidi ya Yanga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...