Naibu Mkurugenzi wa Habari wa Bank M,Allan Msalilwa akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani) katika Ukumbi wa Hayyat Regency ,jijini Dar es Salaam juu ya huduma zinazotolewa na benki hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu Biashara wa Bank M,Jacqueline Woiso akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu uboreshaji wa huduma kwa wateja wa benki hiyo.
======= ======== ======== ===========
Na Chalila
Kibuda na Globu ya Jamii,Dar.
Benki M
imesema imeendelea kuboresha huduma kwa wateja katika uendelezaji wa viwanda
pamoja na mikopo katika miradi ya jamii ikiwepo kudhamini maji.
Akizungumza
na waandishi leo katika Ukumbi wa Hoteli ya Hayyat Regency Jijini Dar es
Salaam,Afisa Mtendaji Mkuu wa Biashara wa Benki M,Jacqueline Woiso ,alisema
kufanya hivyo kuboresha hivyo ni kutaka wateja wa benki M kuendelea kunufaika.
Alisema
mikopo waliositisha ni ya nyumba pamoja na elimu na kufungua milango ya mikopo
kwa taasisi kwa ajili ya maji na viwanda ili kuweza wananchi kunufaika katika
viwanda pamoja na maji.
Jacqueline alisema benki inawakaribisha wateja wapya
kujiunga na benki hiyo ili kuweza kunufaika na huduma mpya zitakazoweza kusaidia
jamii kupata maendeleleo.
Aidha
alisema huduma nyingine ni uwekaji wa mashine ya kukusanyia fedha kutoka kwa
wateja ili kuondoa usumbufu kutoka sehemu moja kwenda nyingine
Tatizo siyo wakweli, wana maneno mazuri sana wanapotaka ufungue a/c, lakini ukishakuwa ndani tu, unakuwa kama mtumwa, as if hawakujui,.. Bank M
ReplyDelete