Embedded image permalink
Na Abou Shatry DMV 


Kama vile matangazo ya hali ya hewa yalivyo tolewa mwazoni mwa wiki hii na National Weather Service, katika maeneo mbali mbali ya hapa DMV kwamba  hali ya hewa itazidi kuwa baridi na kutegemea kuanguka  theluji ya inches mbili hadi tatu  katika maeneo mbali mbali hapa DMV

Theluji hiyo iliotarajiwa kuanguka mapema mapema mida asubuhi 6: AM ya leo Jumanne Jan,6 na kutegemea kusimama kuanguka mida ya 11:AM ya Saa tano mchana . 

Aidha maeneo mbali mbali ya barabara kuu yameonekana kufanyiwa usafi mapema  na magari ya usafishaji kumwagiliaji chumvi maalumu ambazo hupunguza mitelezo inayotokea mara kwa mara wakati theluji hizo zinapotokea kila ifikapo msimu wa baridi.

Pia tunapenda kutoa tahadhari kwa  Madereva wa magari kuwa makini na theluji ambayo husababisha ajali za barabarani  na haswa mnapokuwa katika barabara kuu za Highway na njia za ndani, kwa maana hadi sasa mitelezo na mafoleni baadhi ya maneno mbali mbali yameshaanza kujitokeza katika baadhi ya mabarabara Ndani ya DMV kwa hiyo tunawaomba waTanzania wote wanaoishi maeneo yaliokubwa na theluji hiyo kuwa makini wakati unapoendesha gari lako.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Aaaaah! Nilikuwa sina habari. Ntahakikisha nakuja hapa kupata hali halisi ya hali ya hewa.

    ReplyDelete
  2. Watanzania jifunzeni kiswahili sanifu,hiyo iliyoanguka huko DMV na inayoendelea kuanguka kota Marekani na Canada na mahali pengine duniani palipo na kipupwe (winter) kwa sasa ni THELUJI (snow) na siyo BARAFU (ice) kama ulivyosema mdau uliyeleta tangazo hili la kuanguka kwa theluji(snow) huko DMV-Marekani.

    ReplyDelete
  3. Hiyo sio "barafu"... ni "theluji"

    barafu ni "ice" hiyo ni "snow" kwa lugha ya kiingereza.

    Tujishughulishe..!!

    ReplyDelete
  4. DMV ndio wapi

    ReplyDelete
  5. Raha yote ya ulaya huishia kwenye baridi kali, siku mfupi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...