Sikiliza hapo chini taharuki ya panya Road ilivyozua tafrani na hofu kubwa kwa maeneo mbalimbali ya wakazi wa jiji la Dar. Baadhi ya Wadau walikumbana Live na rabsha hiyo ya Panya Road
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum jijini Dar,Kamanda Kova akitoa ufafanuzi wa habari za taharuki katika vyombo vya habari hususani televisheni,kuhusiana na sakata la kundi la Vijana wajiitao Panya Road,amesema suala hilo lilikuwa dogo,lakini baadhi ya watu wamelikuza na kupelekea hofu kubwa kwa Wananchi ''Jiji mpaka sasa liko salama na wananchi watulie wasiwe na hofu kwa sababu jeshi la Polisi liko imara kuhakikisha amani inakuwepo ya kutosha,na hao vijana hawawezi kulishinda Jeshi la Polisi'',alisema.Alisema Wananchi waondoe hofu waendelee na shughuli zao kama kawaida.
 katika hali isiyo ya Kawaida na ya kuogopesha,kumeibuka taharuki kubwa usiku huu kwa Wakazi wa maeneo mbalimabali ya jiji la Dar,ikiwemo,Sinza,Kinondoni,Mwananyamala,Mabibo,Magomeni,Manzese,Kagera na Mburahati kwa kile kinachoelezwa kuwa vijana waitwao Panya Road wamevamia maeneo hayo na kuwajeruhi watu kwa vitu vyenye ncha kali,visu na mapanga na kuwapora vitu (mali zao) walivyokuwa navyo,kama vile haitoshi baadhi yao wamevunjiwa vioo vya magari yao.
Chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa vijana hao waitwao Panya Road wameibuka na kufanya uhalifu huo mara baada ya tukio la Mwenzao mmoja kudaiwa kuuwawa na Polisi.

Aidha Chanzo hicho kimebainisha kuwa baada ya taarifa kusambaa kwa haraka,kimeeleza kuwa Jeshi la Polisi limeingia kazini kuwasaka watuhumiwa hao walioibua tafrani kubwa usiku huu. 

Wadau tutazidi kuwaletea taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo kadiri ya zitakavyokuwa zikipatikana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kama his taarifa ni za kweli ni hatari.Tunaomba jeshi la polisi na ikiwezekana jeshi la kujenga taifa waingilie kati kwani magenge kama haya ni hatari kwa kila raia. Wadhibitiwe kwa njia yoyote ile kabla ugonjwa wao haujasambaa sehemu nyingine.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...