Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii asubuhi hii,inaeleza kuwa majambazi yamevamia kituo cha Polisi cha Ikwiriri, Rufiji mkoani Pwani na kuua Askari wawili na kupora silaha (bunduki) zilizokuwepo kituoni hapo.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo,huku askari wanaodaiwa kupotenza maisha ni Cop. Edgar  aliyekatwa mapanga na Wp Judith aliyepigwa risasi ubavuni upande wa kulia na kutokea upande wa kushoto.

 Hivi sasa hali ni tete katika eneo hilo na watu wamekusanyika huku polisi wakiongeza nguvu kusaka wauaji katika Tukio la uvamizi, kituo cha polisi Ikwiriri, Rufiji, Pwani

Silaha zilizoporwa ni SMG 2, SAR 2, SHORTGUN 1, silaha 2 za mabom ya machozi na risasi 60 za smg.

tutaendelea kujuzana kadri taarifa zitakavyokuwa zikitufikia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mambo gani haya jamani. Wanaohusika wachukue hatua ili polisi wapewe usalama zaidi na matukio kama haya ya uvunjifu wa sheria na amani yasitokee tena.

    ReplyDelete
  2. Kisha kuna wajinga wanatuambia eti tuondoshe hukumu ya kifo!!! Adhabu ya makosa kama haya itakuwa nini?

    ReplyDelete
  3. Occupational hazzard, Mwenyezi Mungu awalaze mahali pema peponi.

    ReplyDelete
  4. Duu hii mijambazi mi siipendi

    ReplyDelete
  5. Kwanza Nawapa pole familia za marehemu kwa kufiwa na ndugu zao.

    Pili, Watu wanatakiwa Wajiuzuru ndani ya jeshi la polisi maana huu ni uzembe mkubwa kwa kumbukumbu zangu inatokea mara mbili sasa baada ya ile ya Bukombe wakati huohuo tunasikia mara songea na Arusha milipuko...Kituo cha Polisi ni kama ngome ya kijeshi, inatakiwa ijiweke kikamilifu wakati wote dhidi ya mashambulizi na ukiona mashambulizi yanatokea mara kwa mara basi ujue kuna tatizo kwenye Chain of command ya kijeshi ktk vitengo vyao vyote...Jeshi imara ni lile linaloweza kuzuia tukio kabla halijatokea na inabidi wakati ufike kwa Tanzania kukubali kukosolewa ata kama hatupendi kusikia au kushauriwa na wahusika wajiuzuru na kukubari makosa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...