Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ambao Serikali ya Tanzania imeanza kuutekeleza tangu Julai, 2013 umeleta matokeo makubwa yatakayosaidia kukuza uchumi wa nchi na huduma kwa wananchi.
Hayo yalisemwa juzi visiwani Zanzibar na Mtendaji Mkuu kutoka Ofisi ya Rais-Usimamizi wa Utekeleaji wa Miradi (PDB) inayosimamia utelezaji wa BRN kwa Tanzania Bara, Omari Issa alipokuwa akitoa mada kwa watendaji waandamizi wa Serikali.
Katika semina hiyo iliyohudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein, Mawaziri, Makatibu Wakuu na viongozi wengine waandamizi wa Serikali, Bw. Issa alieleza uzoefu wa mwaka mmoja wa utekelezaji wa BRN Tanzania Bara.
Bw. Issa alisema mafanikio ya BRN kwa Tanzania Baya yametokana na nidhamu ya utendaji ambayo mfumo huo umeileta ikiwemo kuweka vipaumbele vichache vinavyogusa sekta muhimu kwa Taifa, kuweka muda na mfumo wa utekelezaji ili kupata matokeo ya haraka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...