Waendesha Daladala jijini Arusha,leo wamefanya mgomo wa kutoa huduma ya kusafirisha abiria katika maeneo mbali mbali ya mji huo kwa kile kinachodaiwa kugomea kuanzishwa kwa route mpya wanayotakiwa kuianza hivi sasa. 

Wakazi wa maeneo mengi ya jiji hilo wanalazimika kutembea kwa miguu,huku wengine wenye uwezo kidogo wakitumia  usafiri wa bodaboda ili kuwahi katika shughuli zao za kuendelea kujitafutia chochote.Askari Polisi na migambo wamesambaa kona za njia zote jijini Arusha.

Route zenye mgogoro zaidi ni ile ya Kutoka Njiro na Moshono kuelekea mjin.

Ripota wetu ambane nae ni mhanga wa mgomo huo,anasema kuwa angalau hali ya hewa leo inaruhusu kutembea bila kuchoka na Bodaboda hazijazuiwa kufika katikati ya mji wa Arusha,hivyo zinasaidia usafirishaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Naunga Mkono mabadiliko ya Route,Hiace zilikuwa kero mitaa ya mjini kati,Cha msingi wamiliki wa Daladala hawaja tumia akili kwa kutesa wananchi wasio na Hatia,Wao wanatakiwa waka toa hoja zao kwa Serikali ya Mkoa,
    Cha kushangaza wakati wa mikakati ya kubadilishwa kwa route inafanyika Wamiliki na Wajumbe wao wali Afikikiana ktk mabadiliko yote haya iweje leo wagomee? " MABADILIKO KATIKA MAISHA YA MWANADAMU HUWA MAGUMU MWANZONI"

    ReplyDelete
  2. Sumatra msiwabembeleze hawa jamaa kama hawataki waanze waje wengine!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...