Na JOHN DOTTO,  Mwanza 
 WAZIRI wa Ujenzi Dkt. John Magufuli ameagiza kufungwa kwa mfumo mpya wa kielektroniki katika vivuko vyote nchini ili kukabiana na wajanja wachache wanahujumu mapato katika vivuko hivyo. 
 Mbali ya hilo, ameagiza kufanywa kwa utaratibu utakaowezesha huduma katika vivuko zinatolewa kwa saa 24 ili kukidhi mahitaji ya wananchi. 
 Dkt. Magufuli alitoa maagizo hayo jana katika uzinduzi wa mfumo mpya wa kielektroniki katika kivuko cha Kigongo -busisi mkoani hapa uliowekwa na Kampuni ya Africom Tanzania. 
 "Tulianze pale Kigamboni na tukaona mafanikio, tulipokuja hapa (Kigongo) tukaboresha na mafanikio yameonekana kwa kiasi kikubwa. Vivuko vyote sasa vifungwe mfumo mpya wa kielektroniki...vivuko vyote nchini," aliagiza Dkt. Magufuli. 
 Alisema mfumo huo una faida kubwa ikiwemo kudhibiti upotevu wa mapato ambapo katika kivuko cha kigongo - Busisi alisema mapato yameongezeka kwa takribani asilimia 40 baada ya kufungwa kwa mfumo huo. 
 Hata hivyo, Dkt. Magufuli alikataa kutaja ni kwa shilingi ngapi mapato hayo yameongezeka kwa hofu kuwa watu wenye dhmira mbaya wakisikia wanaweza kwenda na kufanya uhalifu. 
 Pia, aliagiza Kivuko kwa Kigamboni nacho kiboreshwe mfumo wake kama ilivyokuwa kwa Kigongo - Busisi. Waziri huyo wa Ujenzi, alisema kutokana na mafanikio yanayopatikana katika kudhibiti upotevu wa mapato na kurahisisha huduma kwa wananchi, wafanyakazi husika kwa maana ya wale wa TEMESA maslahi yao yanapaswa kuangaliwa upya na kuboreshwa. "Kama mapato ni mazuri, wafanyakazi nao walipwe vizuri, wasikae kimasikini kwani wanapaswa kuona mwaka 2015 ni ukombozi katika maisha yao. 
 Alisema serikali chini ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete imefanikiwa kujenga madaraja yote makubwa nchini ambapo kwa sasa kuna madaraja 4880 nchini na kuwa wakati inapata uhuru kulikuwa na madaraja mawili ambayo yalikuwa ya kuvutwa. 
 Mfumo wa kielektroniki katika vivuko vya Kigamboni na Kigongo Busisi ulifungwa na Kampuni ya Africom Tanzania ambaye Mkurugenzi Mtendaji wake Juma Rajabu alisema watahakikisha wanafunga mifumo ambayo itadhibiti upotevu wa mapato na kurahisisha huduma kwa wananchi ambao ndiyo watumiaji.
Dkt. John Magufuli akikata utepe kuzindua  mfumo mpya wa kielektroniki katika kivuko cha Kigongo -busisi mkoani hapa uliowekwa na Kampuni ya Africom Tanzania.
Dkt. John Magufuli akikata utepe kuzindua  mfumo mpya wa kielektroniki katika kivuko cha Kigongo -busisi mkoani hapa uliowekwa na Kampuni ya Africom Tanzania.
Dkt. John Magufuli na viongozi wa mkoa wa Mwanza wakifurahia baada ya kukata  utepe kuzindua  mfumo mpya wa kielektroniki katika kivuko cha Kigongo -busisi mkoani hapa uliowekwa na Kampuni ya Africom Tanzania.
Mfanyakazi wa  kivuko cha Kigongo -busisi mkoani Mwanza akionesha wananchi namna ya kutumia mashine hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Sahihisho: Kampuni iliyosimika mfumo wa elektroniki Kigongo Busisi inaitwa Maxcom Africa limited na si africom Tanzania. Hongereni Temesa kwa mafanikio haya.

    ReplyDelete
  2. Sahihisho: taarifa ya waziri ni kuwa kwasasa kuna vivuko takiribani thelathini (30) nchi nzima. Kabla ya uhuru tulikuwa na vivuko viwili (2) na vilikuwa vinavutwa kwa kamba.na si kwa sasa kuna madaraja 4880 nchini na kuwa wakati inapata uhuru kulikuwa na madaraja mawili ambayo yalikuwa ya kuvutwa.

    ReplyDelete
  3. Tatizo hata mkifunga mitambo ya kielectronic bila close monitoring inakuwa wizi mtupu. Mfano Kigamboni huwa wanakusanya issued ticket then wanaziuza tena sasa fikiria kwa siku wanaiba ngapi??? please watch out mana Serikali inapoteza sana mapato kwa wajanja wachache. Hapo ni ticket bado wizi wa mafuta....Ni shideer

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...