Salaam Ankal na Timu nzima ya Globu ya Jamii

Nawasilisha picha mbili zilizopigwa kutoka Mazengo Street, Upanga (Chibuku, Faya),maana naona hawa Jamaa wa RAPID wanatupotosha na tukikosea trafiki wanatupiga faini. Tufanyeje?
kwa mfano,picha hii inaonyesha hakuna kuingia Morogoro Road Kuelekea Ubungo.Alama ya Barabarani inaelekeza magari yote yanayotoka Mazengo kwanza lazima yanyooshe kwenda Barabara ya Msimbazi na baadae kuingia Morogoro Road kufuata mshale inavyo onyesha hapo pichani,wakati ukielekea Msimbazi hakuna sehemu ya kuingia kushoto ili uje kutokea Morogoro Road.

Na kuna alama nyingine mbele kidogo na hapo inayoelekeza namna ya kuingia Mazengo Street kwenye barabara kuu ya Morogoro Road ambayo haieleweki vilevile (Sikuweza kuipiga picha).

Picha hii ya pili inaonyesha Alama ya kwenda Swahili Street huku mshale unaelekeza kwenda Mazengo Road, Sasa hiyo Swahili Street iko wapi huko Upanga? Na kama Mazengo Street imebadilishwa jina,imebadilishwa Lini?

Ni hayo tu Ankal kwa leo,Naomba Msaada tutani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...