Hashim Kambi ‘Ramsey’
 Msanii mkongwe katika tasnia ya filamu za Bongo Movie Hashim Kambi ‘Ramsey’ ni moja kati ya wasanii wakubwa Bongo ambaye atawaongoza wasanii nyota na wakongwe katika filamu kubwa ya CPU inayotarajiwa kuingizwa katika DVD baada ya kuonyeshwa katika majumba ya sinema ndani na nje ya nchi.

Filamu ya CPU ni moja ya kazi kubwa sana kutengenezwa na watayarishaji wa ndani na kushirikisha wasanii zaidi ya 200 na  ni filamu  yenye ubora wa kipekee ambayo awali ilionyeshwa katika ukumbi wa sinema Century Cinemax Mlimani City jijini Dar es salaam kwa siku 10 mfululizo na kuacha gumzo kwa wapenzi wa sinema.
Dude
Kwa mara ya kwanza itauzwa katika DVD kwa wapenzi wa filamu walioshindwa kuingia katika majumba ya sinema ilipoonyeshwa  ili waweze kushuhudia teknolojia ya hali ya juu kutumika Bongo na kuwavutia wengi mtaani kwetu ambako ndio soko la filamu za kibongo lilipo.
CPU inawakutanisha wasanii nyota na wakongwe na Kulwa Kikumba ‘ Dude’, Richard Mshanga ‘Masinde’, Dotnata, na nyota wengine kibao ambao wanafanya vizuri katika tasnia ya filamu wakiongozwa na Hashim Kambi ‘Ramsey’ msanii aliyejijengea mashabiki wengi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...