Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutubia katika mkutano ulioandaliwa rasmi kuwaambia wananchi wa Mponde, Halmashauri ya Wilaya ya Bumburi, Lushoto mkoani Tanga, kuwa Rais Jakaya Kikwete amekubali kukirudisha Kiwanda cha Chai cha Mponde kwa wananchi baada ya mgogoro dhidi mwekezaji wa kiwanda hicho, Yusufu Mula uliodumu kwa takribani miaka 10 na kusababisha kiwanda hicho kufungwa maiaka miwili iliyopita na kuwaacha wananchi kwenye lindi kubwa la umasikini.

Hayo ni Mafanikio ya Katibu Mkuu wa CCM,  Abdulrahman. Kinana ambaye katika mkutano wa hadhara uliofanyika Septemba mwaka jana katika Kijiji cha Mponde, aliahidi kupata suluhu ya mgogoro wa kiwanda hicho ulioshindikana kutatuliwa kwa muda mrefu kwa kuupeleka kujadiliwa katika Kamati Kuu ya CCM na kupata ufumbuzi ndani ya mwezi mmoja, ahadi ambayo aliitimiza.

Kiwanda hicho kilifungwa baada ya wananchi kususia kuendelea kulima mashamba ya chai kwa lengo la kuishinikiza Serikali kutatua haraka mgogoro dhidi ya Mwekezaji wa kiwanda hicho, Yusufu Mulla, ambaye walidai kuwa alikuwa anawanyanyasa wakulima wa zao hilo pamoja na wafanyakazi kuwalipa ujira mdogo.

Kinana amesema Serikali itanunua hisa za mwekezaji ili aondoke na kuwaachia wananchi kiwanda hicho.Pia Serikali itatuma jopo la wataalamu watakao tathmini hasara iliyopo, na kutafuta mtaji wa kukifufua kiwanda  ili kianze kufanya kazi
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli,Mh. January Makamba akiishukuru Serikali kwa uamuzi wake wa kukirudisha kiwanda hicho kwa wananchi ambapo pia alimshukuru Rais Jakaya Kiwete na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman kwa kufanya jitihada za kuhakikisha wananchi wanapata haki yao hiyo walioisotea kwa takribani miaka 10.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Bumbuli Mh. Januari Makamba wakati alipowasili jimboni humo katika wilaya ya Lushoto, akiwa katika ziara ya siku mbili ambapo amefanya mkutano wa hadhara katika kata ya Mponde na kuwataarifu wananchi na wakulima wa Chai kuhusu maagizo ya Rais Jakaya Kikwete juu ya kukirejesha kiwanda cha Chai cha Mponde kwa wananchi .
 Mkuu wa Wilaya ya Lushoto,Mh.Majid Hemed akizungumza na Wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika kijiji cha Mponde,mkoani Tanga.
 Baadhi ya Wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo wa hadhara wakisikiliza kwa makini.
 Mkutano ukiendelea katika uwanja wa Mponde,katika Halmashauri ya Bumbuli mkoani Tanga jioni ya leo.

PICHA NA MICHUZI JR -BUMBULI-TANGA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...