Kamati ya Bunge ya kilimo, maji na mifugo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Prof. Peter Msola imefanya ziara katika mkoa wa Morogoro kwa kutembelea kijiji cha Fulwe,mradi wa maji wa Mambogo manispaa Morogoro na mradi maji mikumi.
Aidha tarehe 22 Januari ,2015 kamati hiyo itatembelea wilaya ya Kilolo na manispaa ya Iringa na tarehe 23 kamati itatembelea wilaya ya Rungwe.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya kilimo, maji na mifugo,Prof. Peter Msola (shati nyeupe) akiongoza kamati yake kukagaua mradi maji wa Mambogo manispaa ya morogoro.Katikati ni Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla.
Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla (kushoto) akiongea na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya kilimo, maji na mifugo,Prof. Peter Msola walipotembelea mradi maji Mikumi.
Naibu Waziri wa Maji,Mh. Amos Makalla akitoa maelekezo kwa mkandarasi mradi maji Mikumi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...