Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo,Maji na Mifugo Mh. Subira Mgalu (kushoto) akieleza jambo wakati walipoenda kutembembelea
miradi ya Maji kanda ya Kaskazini.
Kamati ya Maji, Mifugo na Uvuvi imeridhishwa na miradi mbalimbali ya Maji iliyotekelezwa kwa kipindi cha miaka 10 ya kuwapatia wananchi huduma ya Majisafi na kupunguza tatizo la uhaba wa Maji hapa nchini.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa kamati ndogo ya Maji Mh. Selemani Kakoso Wakati wa ziara ya kamati katika kuangalia miradi ya Maji iliyofanikiwa katika baadhi ya mikoa ya kaskazini.

Katika ziara hiyo wajumbe wa Kamati walitembelea Mkoa wa Tanga kwa kuanzia wilaya ya Muheza na kutembelea mradi wa maji wa vijiji 10 katika kata ya Ubembe ambapo mradi huo wa Maji umeweza kuwanufaisha wananchi zaidi ya 1600 na hivyo kupunguza kero ya Maji na kuwapa wananchi nafasi zaidi ya kufanya shughuli za maendeleo.
Pia kamati hiyo iliweza kuona uchafuzi wa Vyanzo vya Maji katika mto Zigi na kutoa wito kwa mamlaka ya Maji Tanga pamoja na hifadhi ya bonde la pangani kushirikiana kwa pamoja kuweka usimamizi shirikishi wa pamoja ili vyanzo vya Maji vilindwe kwa ajili ya kizazi hiki na kizazi kijacho.
Mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Muheza, Bi Subira Mgalu aliyekuwepo katika ziara hiyo alitoa wito pia kwa jamiii kuonyesha ushirikiano katika kuwabaini wananchi wanaofanya shughuli za uchimbaji madini katika vyanzo vya Maji kwani wanaojishughulisha na shughuli hizo ni wananchi wa maeneo hayo na si vyema kulindana kwani ili kuleta maana nzima ya ulinzi shirikishi kwa jamii husika
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...